1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UEFA EURO 2012 yaanza

8 Juni 2012

Baada ya ngoja ngoja ya muda mrefu hatimaye pazia la kinyang'anyiro cha kombe la mataifa ya bara la Ulaya yaani UEFA EURO 2012, linapandishwa leo (08.06.2012) huko Ukraine na Poland.

https://p.dw.com/p/15AXm
Die Hände der Maskottchen der Fußball-Europameisterschaft UEFA Euro 2012 Slavek und Slavko halten am Freitag (20.04.2012) in Kiew in der Ukraine in einem Geschäft für lizensierte Fanartikel der Euro EM 2012 Europameisterschaft Polen Ukraine einen Fußball mit dem Logo der Euro 2012. Im Hintergrund der Schriftzug "Official Licensed Product". Foto: Jens Kalaene
Fußball-Europameisterschaft UEFA Euro 2012Picha: picture-alliance/dpa

Lakini wakati mamilioni ya wapenzi wa soka wakitarajiwa kuburudishwa na uhondo wa tamasha hilo ambalo ndilo maarufu zaidi miongoni mwa mashabiki wa Ulaya, kunayo hofu ya kuchafuliwa na visa vya ubaguzi. 

Hata kabla ya kipyenga cha kuanza michuano kupulizwa, tayari kuna madai ya kutokea visa vya ubaguzi wa rangi katika dimba la UEFA EURO 2012 linaloandaliwa Poland na Ukraine. Nahodha wa timu ya taifa ya Uholanzi Mark van Bommel amesema katika mahojiano yaliyochapishwa leo kwamba timu yake ilisikia nyimbo za kibaguzi wakati ikifanya mazoezi ya kikosi mbele ya mashabiki katika mji wa kusini mwa Poland, Krakow.

Uholanzi yalalamika

Van Bommel amenukuliwa na gazeti la De Telegraf akisema kuwa wote walisikia nyimbo za kumwiga tumbili, na hawawezi kukubali hilo. Kiungo huyo wa klabu ya AC Milan aliongeza kuwa ikiwa tukio kama hilo litatokea wakati wa kinyang'anyiro, watamwendea mwamuzi wa mechi mara moja na kumwomba aingilie kati.

epa03250015 (L-R) Dutch national soccer layers Wesley Sneijder, Joris Mathijsen and Dirk Kuyt during a training session at the Reymana stadium in Krakow, Poland, 05 June 2012. The Dutch team is preparing for the UEFA EURO 2012 soccer championship which will take place from 08 June to 01 July 2012 in Poland and Ukraine. EPA/KOEN VAN WEEL +++(c) dpa - Bildfunk+++
Timu ya Uholanzi mazoeziniPicha: picture-alliance/dpa

Afisa mmoja mkuu wa shirika la soka la Ulaya UEFA aliliambia shirika la habari la AFP kuwa kundi dogo la waandamanaji liliulenga uwanja wa mazoezi unaotumiwa na timu ya Uholanzi mjini Krakow siku ya Jumatano lakini akakanusha kuwa maandamano hayo yalikuwa ya kibaguzi.

Rais wa UEFA Michel Platini amewataka waamuzi wa mechi kuzuia au hata kusitisha michuano ikiwa wachezaji watabaguliwa na mashabiki. Shirikisho hilo limemteua refa Muitaliano Nicola Rizzoli kuamua mchuano wa hisia kali kati ya Uingereza na Ufaransa mjini Donetsk mashariki mwa Ukraine siku ya Jumatatu.

UEFA imewaeleza waamuzi wa mechi 12 jinsi ya kushughulikia nyimbo za kibaguzi na ishara kutoka katika maeneo ya viti vya mashabiki.

Mafanikio ya wenyeji

Naye rais wa Ukraine aliwataka wananchi wake kuwakaribisha wageni kwa moyo mkunjufu wakati wa dimba hilo. Rais Viktor Yanukovych alisifu mafanikio yaliyopatikana katika kuandaa kinyang'anyiro hicho. Alipongeza nchi hiyo kwa kujenga barabara, viwanja vya michezo na ndege kwa ajili ya UEFA EURO 2012.

***Das Pressebild darf nur in Zusammenhang mit einer Berichterstattung über die Ausstellung Choreographie der Massen in Berlin verwendet werden*** Olympiastadion Kiew Olympic Stadium, Kiev gmp • Architekten von Gerkan, Marg und Partner Foto © Marcus Bredt Pressefotos zur Ausstellung Choreographie der Massen Im Sport. Im Stadion. Im Rausch 6. Juni – 12. August 2012 Galerie der Künste Berlin Veröffentlichung kostenfrei im Rahmen der aktuellen Berichterstattung zur Ausstellung. Nennung der Credits zwingend erforderlich. Belegexemplar erwünscht.
Uwanja wa KievPicha: Marcus Bredt

Katika mechi za leo mbili za ufunguzi Wenyeji Poland watafungua dimba dhidi ya Ugiriki kabla ya Jamhuri ya Czech kujitosa uwanjani kuvaana na Urusi.

Wakati huo huo Uingereza imesema kuwa haitawatuma mawaziri wowote katika mechi za awamu ya makundi. Ofisi ya mambo ya kigeni ya Uingereza imesema hakuna maafisa wa ngazi za juu watakaohudhuria mechi za awamu hiyo huku kukiwa na ripoti za kufungwa jela Waziri Mkuu wa zamani Yulia Tymoshenko.  Nchi kadhaa za Ulaya ikiwemo Ufaransa na Austria tayari zimetishia kususia dimba hilo zikitaja ripoti za unyanyasaji wa kiongozi huyo wa Upinzani nchini Ukraine aliye gerezani.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Yusuf Saumu