1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufaransa itafanikiwa kuleta amani eneo la Nagorno-Karabakh?

9 Oktoba 2020

Kuna harakati za kutatua mzozo kati ya Azerbaijan na Armenia juu ya jimbo la Nagorno-Karabakh, huku Ufaransa ikishiriki mazungumzo kati ya mahasimu hao wawili.

https://p.dw.com/p/3jhKA
Berg-Karabach Konflikt
Picha: Aris Messinis/AFP/Getty Images

Kwa mujibu wa taarifa kutoka afisi ya rais wa Ufaransa Emanuel Macron, hali iliyopo kwa sasa "bado ni dhaifu sana" baada ya kushiriki mazungumzo kwa njia ya simu yaliyofanyika Alhamisi na Ijumaa.

Rais Macron alizungumza kwa njia ya simu na Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan jioni ya Alhamisi jioni na Ijumaa akawasiliana na Rais Ilham Aliyev wa Azerbaijan.

Taarifa zinasema kuwa Ufaransa imekuwa ikishirikiana na Rais Vladimir Putin wa Urusi tangu mwanzoni wa wiki katika juhudi za kutafuta suluhu juu ya eneo hilo la Armenia lililojitenga na lenye wakaazi wa Kiarmenia.

Urusi, Ufaransa na mwenyekiti mwenza wa kundi la Minsk Group, Marekani, kupitia Shirika la Usalama na Ushirikiano barani Ulaya (OECD) wanaendelea na juhudi za kupata suluhu kwa njia ya amani katika mzozo huo uliodumu miaka mingi.

Jimbo la Nagorno-Karabakh limeshudia mapigano mapya tangu Septemba, huku Ufaransa ikiinyoshea kidole cha lawama Azerbaijan ambayo inaungwa mkono na Uturuki katika mzozo huo.

Awali wanadiplomasia wakuu wa kutoka pande zote mbili walikuwa wakikutana mjini Moscow hata kabla ya machafuko hayo hayajatoa ishara yoyote ya mapatano.

"Tunaelekea kwenye makubaliano usiku wa leo au kesho lakini bado ni dhaifu," kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa afisi ya Rais Emmanuel Macron ilisema katika taarifa kwa AFP.

Mawaziri wa maswala ya nje wa Armenia na Azerbaijan wamealikwa mjini Moscow na Rais Putin.