1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufaransa yataka kujerea katika jumuiya ya NATO

Charo Josephat/ Hasselbach, Christoph4 Machi 2009

Ufaransa yataka kuwa mwanachama kamili wa muungno huo wa kijeshi

https://p.dw.com/p/H5hW
Rais wa Ufaransa Nicolas SarkozyPicha: AP

Pengine umewadia wakati wa ukweli kujidhihirisha tena. Baada ya miaka 43 Ufaransa inataka kuwa mwanachama kamili wa jumuiya ya NATO. Waziri wa ulinzi wa Ufaransa Hevre Morin amesititiza siku ja Jumanne kwamba kurejea kwa nchi hiyo kwa jumuiya ya NATO hakutaathiri misingi ya uhuru wa Ufaransa. Ufaransa itawasilisha ombi la kurudi katika jumuiya ya NATO mwezi Aprili mwaka huu wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 60 tangu kuasisiwa jumuiya hiyo.

Mnamo mwaka 1949 Ufaransa ilikuwa miongoni mwa wanachama walioasisi jumuiya ya kujihami ya kambi ya magharibi NATO na ikashikilia makao makuu ya jumuiya hiyo. Lakini rais Charles de Gaulle akuwa na wasiwasi na uwezo mkubwa wa Marekani tangia mwanzo. Wakati Ufaransa ilipoanza kuwa na nyuklia kiongozi huyo hakutaka uamuzi kuhusu silaha za nyuklia awaachie wengine. Mnamo mwaka 1966 akaamua kujiondoa kutoka kwa muungano huo wa kijeshi.

"Inahusiana na kurejesha tena hali ya kawaida ya utaifa´"

Makao makuu ya jumuiya ya NATO yalihamishwa kutoka mjini Paris hadi Brussels Ubelgiji. Ufaransa ingeweza kuamua peke yake kuhusu maswala ya nyuklia, lakini ikapoteza ushawishi katika jumuiya ya NATO. Uamuzi huu uliendelezwa na marais wengine waliomtangulia kiongozi huyo. Wakati wa uvamizi wa Irak mnamo mwaka 2003 ulioongozwa na Marekani, mjadala kuhusu uhusiano kati ya Marekani na Ulaya ukapata muamkao mpya.

Rais wa zamani wa Ufaransa, Jacquis Chirac anasema, "Hatuoni sababu yoyote kubadili wazo letu. Ni wazo la amani na ni mojawapo ya mawazo yanayoweza kuzuia kutokea kwa vita"

Ni kweli kwamba katika miaka ya 1990 mawazo yalianza kubadilika nchini Ufaransa. Kumalizika kwa vita baridi kulisababisha hali mpya kutokea. Na tangu mwaka 2001 vita dhidi ya ugaidi vimeongeza shinikizo zaidi. Sasa rais Nicholas Sarkozy wa Ufaransa anataka kuirejesha nchi hiyo kuwa mwanachama kamili wa jumuiya ya NATO.

Ukweli ni kwamba Wafaransa wengi wana shakashaka, lakini rais Sarkozy anahoji akisema, "Barani Ulaya karibu washirika wetu wote ni wanachama wa jumuiya hii. Na hawaelewi kwa nini sisi bado tunaendelea kukaa nje ya uanachama wa jumuiya hii."

Rais Sarkozy anaelewa kuirejesha Ufaransa katika NATO hakutaidhoofisha nchi hiyo bali kutaiimarisha. Amewahi kusema Ufaransa itakuwa na vyeo muhimu katika jumuiya hiyo. Lakini rais Sarkozy hataki tu kuiimarisha Ufaransa pekee, lakini kuiimarisha pia jumuiya ya NATO. Ingawa Ufaransa si mwanachama wa NATO, imeshiriki katika tume za jumuiya hiyo nchini Afghanistan na katika mataifa ya Balkan.

"Yote kwa pamoja. Ulaya inayojitegemea katika maswala ya ulinzi na jumuiya ya kujihami ya NATO. Katika jumuiya zote mbili tutachukua nafasi yetu."

Rais Sarkozy hazungumzii jumuiya ya NATO ya wazungu kwa Wafaransa tu bali pia kwa washirika wake Ulaya hususan Ujerumani.

Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Franz Josef- Jung kwenye mkutano wa jumuiya ya NATO mjini Krakau nchini Poland mwezi uliopita alisema, "Nadhani ingesaidia kama Ufaransa haitakuwa tena tu mwanachama kamili wa jumuiya ya NATO, bali pia Ulaya, ikiwa Umoja wa Ulaya utaendeleza kwa ukakamavu sera zake za ulinzi na kuweza kushauriana kikamilifu na jumuiya ya NATO. Angalia Afghanistan, angalia Kosovo. Huko ni muhimu sana kwamba jumuiya ya NATO na Ulaya zishirikiane kwa karibu sana."

Hivyo ndivyo inavyoonekana. Kurudi nyumbani kwa mwana mpotevu kwenye mkutano wa jumuiya ya NATO utakaofanyika mwezi Aprili mwaka huu, hakuwezi kusubiri tena.