1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ugiriki yakabiliana na mafuriko

10 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD4F

Serikali ya Ugiriki imetangaza hali ya dharura katika maeneo ya kaskazini na kati kati mwa nchi kutokana na mvua kubwa zilizonyesha mwishoni mwa wiki. Vijiji kiasi ya 10 vimekumbwa na mafuriko na ndege za helikopta zimekuwa zikijaribu kuwaokoa watu walionasa katika mafuriko hayo ambayo yamepelekea hata kuvunjika daraja kubwa linalounganisha miji ya Thessalonika na Kavala. Hadi sasa mtu moja hajulikani alipo. Waziri mkuu, Costas Karamanlis, ameahidi fidia kwa wahanga wa mafuriko hayo. Lakini bado wasi wasi upo kwani nvua kubwa zinatarajiwa kupiga kando kando mwa mji mkuu Athens.