1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uhariri:Ziara ya Trump haina tija kwa Uingereza

Saumu Mwasimba
5 Juni 2019

Amependekeza kwamba waziri wa zamani wa mambo ya nje Boris Johnson kutwaa nafasi ya waziri mkuu na Nigel Farage ashirikishwe kwenye mazungumzo na Umoja wa Ulaya.

https://p.dw.com/p/3Jrv0
Großbritannien US-Präsident Donald Trump & Theresa May, Premierministerin
Picha: Reuters/S. Rousseau

Ziara ya rais wa Marekani nchini Uingereza ilikuwa ni sawa na sherehe iliyokosa tukio.Inawezekana kwamba familia hiyo ya Donald Trump imefurahia ziara hiyo katika kasri la kifalme walikopokelewa na Malkia Elizabeth wa pili. Trump alipata nafasi ya kujieleza umuhimu wake,lakini ili iweje au kwanini? Maana hata kilichojitokeza inaonesha hakuna aliyempatiliza anasema Bernd Riegert katika uhariri wake.

Malkia Elizabeth wa pili hajawahi kuzungumzia hisia zake kuhusu hiki wala kile cha mgeni  yoyote wa ngazi ya juu.Kitu ambacho kwahakika ni bahati mbaya.Ingekuwa kitu cha kufurahisha kuona ni kitu gani angeweza kukieleza juu ya anavyomuangalia rais Donald Trump.

Huyu ni kiongozi wa 12  wa nchi wa Marekani kukutana na kiongozi aliyekaa muda mrefu katika ufalme wa Uingereza. Na ni mmoja wa viongozi watatu tu waliowahi kupokelewa kwa heshima kubwa kabisa katika ziara hiyo ya kiserikali. Malkia kama walivyo raia wengi wa Uingereza si hasha wamejiuliza kwanini  Trump kati ya marais wote wa Marekani ndiye aliyepewa heshima hii.

Lakini huenda hata jibu ya swali hilo hakuna,na hasa kwasababu ziara yake haijafanya chochote cha kuiunganisha nchini hiyo ambayo iko katika mgawanyiko mkubwa kuhusu Brexit. Trump wala hakuona aibu kujizuia kuhusu kutoa ushauri juu ya vipi anavyohisi Uingereza inapaswa kuongozwa.

Amependekeza kwamba waziri wa zamani wa mambo ya nje Boris Johnson anapaswa kutwaa nafasi ya waziri mkuu na kwamba rafiki yake wa siasa za kizalendo Nigel Farage ajumuishwe katika mazungumzo ya Umoja wa Ulaya.

Lakini licha ya ukweli kwamba hakuna mazungumzo yaliyopo na Umoja wa Ulaya,kutowa ushauri wa aina hiyo ni kebehi na dharau kubwa kwa waziri mkuu wa sasa Theresa May,hata kama ni mpita njia anayejiandaa kukiachia kiti hicho mwishoni mwa Julai.

Isitoshe ushauri wa Trump wa kuwataka Waingereza waondoke Umoja wa Ulaya bila makubaliano au kile kinachoitwa Hard Brexit,na kuupiga teke Umoja wa Ulaya unakinzana kabisa na msimamo wa Theresa May.

Proteste gegen Donald Trump in London
Picha: Getty Images/AFP/T. Akmen

Wakati fikra ya kumualika rais Trump kuitembelea Uingereza ilipotolewa,wabunge mjini London walitarajia ataweza kujadiliana na nchi hiyo kuhusu mpango wa kibiashara wa baada ya Brexit. Lakini mpaka wakati huu hakuna Brexit.Na hiyo inamaanisha makubaliano yoyote kati ya nchi zote mbili Uingereza na Marekani yatabakia tu kuwa fikra tupu.

Baada ya kukutana na Theresa May rais huyo wa Marekani ameonekana kusisitiza kwamba hatojadili juu ya makubaliano ya kibishara kwa gharama yoyote na kusema makubaliano yoyote yatakayojadiliwa lazima yajumuishe suala la Uingereza kukubali kwa mfano uingizwaji wa bidhaa za kilimo za Marekani na huduma za matibabu.

Na si hilo tu lakini Uingereza kama ilivyo nchi yake Marekani iridhie kuwa tayari kutojihusisha na kampuni kubwa ya kichina ya technolojia ya Huawei sambamba na kujitenga na mkataba wa Nuyklia wa Iran. Haya lakini siyo waliyoyataka wanaounga mkono Brexit nchini Uingereza.

Taratibu wanaanza kuzinduka kuuona dhahiri ukweli kwamba Trump huenda anataka kutumia suala la biashara kama njia ya kuwashinikiza waingereza waliogawika kufanya maamuzi ya kisiasa na kwamba huenda akawekea vikwazo vya kibiashara,kama anavyo fanya kwa China ikiwa haitoafikiana nae. Trump anaufahamu fika udhaifu wa Uingereza na inavyoonesha amejiweka tayari kabisa kuutumia udhaifu huo.

Mwandishi: Bernd Riegert/Saumu Yusuf

Mhariri:Sekione Kitojo