1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uhuru wa vyombo vya habari Kenya

1 Mei 2007

Tarehe tatu mwezi mei ni siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari. Tunaiangalia ripoti ya mwaka 2007 juu ya uhuru huo nchini Kenya.

https://p.dw.com/p/CHF3
Picha: DW

Mwaka elfu mbili na sita ulikuwa mwaka wenye matatizo mengi kwa vyombo vya habari. Migogoro baina yao na mkono wa sheria ilizidi wakati wa kura ya maoni ya katiba,wakati mkewe rais Mwai Kibaki alpoiripotiwa kumnyanyasa mwaandishi habari na waandishi habari wengi kukamatawa kwa madai ya kukiuka sheria.

Mwezi Februari waandishi habari wa gazetti moja la weekly Citizen David Mathenge,Charlse Mwangi na John Wafula walifunguliwa mashtaka na mahakama na kushtakiwa kwa kutowasilisha magazetti yao kwa msajili wa vitabu na magazeti nchini Kenya. Walidaiwa kuchapisha gazeti lao bila leseni na wauzaji magazeti mia moja waliokuwa wakiyauza wakamatwa.

Mwezi huohuo wa februari wandishi habari wengine wa gazzeti la Standard walikamatwa na kuhojiwa baada ya kuchapisha ripoti iliyofichua njama za kisiasa katika serikali. Lakini kilele cha unyanyasaji wa haki za vyombo vya habari kilikuwa tarehe mbili Mwezi Machi ambapo polisi walivamia kituo cha kuchapisha magazeti ya standard na kituo cha televisheni cha Standard KTN na kukifunga.

Maafisa hao wa polisi walikivamia kituo cha KTN saa za machweo na kufunga matangazo yake,wakati huo huo kundi jengine la maafisa hao lilivamia kituo cha kuchapisha magazeti ya standard na kuharibu mitambo yake,wakachoma magazeti yaliokuwa yamechapishwa na kuchukua kompyuta zilizokuwepo. Uvamizi huo uliendeshwa na kundi lijulikanalo kama ,’’kanga’’ ambalo ni kundi lililoundwa na mkurugenzi wa ujasusi makhsusan kwa kukabiliana na wahalifu wa wizi wa magari,benki na wauauaji.

Uvamizi huo unadaiwa kusababishwa na taarifa iliyochapishwa na Sandard ikisema kuwa rais Mwai kibaki alikutana kisiri na kiongozi mmoja wa upinzani.Na shirika hilo likavamiwa siku mbili baada ya onyo kutolewa na serikali kuhusu taarifa hiyo. Wiki mbili baadayew mpiga picha wa shirika hilo eustace Kathurima alikamatwa na watu wanne waliojitambulisha kama maafisa wa polisi na kumeleza alikuwa anachunguziwa kuhusi ulaghai wa vyeti vitatu vya ardhi. Walitia pingu na kuisaka nyumba yake. Muda mfui baadaye walimwachilia kwa madai kuwa walimfananisha na mtu mwengine.

Kamati ya sheria na ya bunge ilimtaka waziri wa usalama John Michuki kuelezea visa hivyo dhidi ya waandishi habari. Na waziri huyo hakusita kusema kuwa hawakuwa na budi ila kutekeleza wajibu wao kwani walipata ripoti kuwa shirika la habari la standard group walitaka kuchapishi taarifa ambazo zingehatarisha usalama wa nchi. Na nikimnukuu Waziri John Michuki alisema ``ukichokoza nyoka itakuuma``

Miezi mwili baadaye shirikla redio la Hope FM linalomilikiwa na kanisa la Pentecosti,nalo likavamiwa,mtu mmoja aliuwawa na wengine watatu kujeruhiwa vibaya . watu watisa walivamia kituo hicho,wakampiga risasi mlinda mlango na kurusha mabomu ya petroli yaliosababisha moto mkubwa kuwaka.

Naye mkewe rais Lucy Kibaki akajikuta katika pakacha la kuwanyanyasa waandishi habari baada ya kumpiga kofi mpiga picha mmoja Clifford Derrick na kuharibu machini yake. Na Mpiga picha huyo alipompeleka mahakamani mkewe rais alipata vitisho dhidi ya maisha yake kesi yake kusambaratika kortini na kulazimika kukimbilia Afrika Kusini anakoishi sasa.

Kesi hizi zimeibua swala la ikiwa serikali inataka kuhakikishia taifa usalama wake kwa kuzia ripoti kuchapisha au inalinda maslahi yake kwa kukomesha ufichuzi wa njama zake. Na mwaka huu ambapo waandishi habari nchini humo watakuwa wanaadimisha uhuru wao, visa hivi vitakuwa kumbukumbu ya kujshinikiza usalama wao kupitia uundaji washeria mwafaka zitakazowalinda kutokana na serikali.

Isabella Mwagodi