1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uingereza kujitoa kutoka Umoja Ulaya bila makubaliano

Sekione Kitojo
30 Machi 2019

Wabunge wa Uingereza wamekataa makubaliano ya Brexit ya waziri  mkuu Theresa May kwa mara ya tatu Ijumaa, na kuashiria uwezekano wa kujiondoa katika mtafaruku katika siku ambayo ingekuwa hasa ya Brexit.

https://p.dw.com/p/3FvSU
Großbritannien London - Debatte zum Brexit
Picha: picture-alliance/dpa/PA Wire/House of Commons

Uamuzi wa  kuukataa mpango uliofupishwa  kidogo wa  makubaliano ya  talaka  kati ya  May  na  Umoja  wa  Ulaya imeliacha suala  la kujitoa kutoka  Umoja  huo  katika  hali  ya  sintofahamu  kwa sasa, lini  na  ama  hata  iwapo  Uingereza  itajitoa  kutoka  Umoja  wa ulaya, na  kulitumbukiza suala  hilo  la mzozo wa  Brexit lililodumu kwa  muda  wa  miaka  mitatu  sasa  katika kiwango kikubwa cha kutoeleweka linaelekea  wapi.

Großbritannien London - Debatte zum Brexit
Waziri mkuu wa Uingereza Theresa MayPicha: picture-alliance/dpa/PA Wire/House of Commons

Waziri  mkuu  wa  Uingereza  Theresa May  anapaswa  kujiuzulu mara  moja  baada  ya  kufanya  majadiliano  ya  muda  ya kurefusha  uanachama  wa muda  wa  Uingereza  katika  Umoja  wa Ulaya , gazeti  la kila  siku  la  Telegraph limesema  katika  toleo  lake la  leo  Jumamosi.

"Hapaswi  kuona , ama  kupaswa  kuambiwa , kwamba  wakati anaweza  kukutana  na  Umoja  wa  Ulaya  kujadili kurefushwa  kwa Brexit, ni  kitu  cha  kawaida  kwamba  ndio  amefika  mwisho  wa barabara. Ni  lazima  ajiondoe, kwa  ajili  ya  Brexit, kwa  chama chake  na  demokrasia  yenyewe," gazeti  hilo  liliandika  katika uhariri  wake.

Gazeti  la  Telegraph  limekuwa  kimsingi  kama  gazeti linalopendelewa  na  wanachama  wa  chama  cha  May  cha Conservative.

Hata  hivyo uwezekano  wa  kuwa  na  waziri  mkuu  mpya  kuongoza awamu  ijayo  ya  majadiliano  ya  Brexit  ilikuwa  haitoshi  kuweza kuwavutia  wabunge  jana  Ijumaa, baadhi  yao  wakihofia makubaliano  yake yanaiacha  Uingereza  ikifungwa  katika  Umoja wa  Ulaya  iwapo  mazungumzo  ya  hapo  baadaye  ya  biashara yatavunjika.

Großbritannien Londom - Debatte im House of Commons
Bunge la Uingereza katika mjadala wa BrexitPicha: picture-alliance/PA Wire/House of Commons

Changamoto kutolewa  madarakani

May, ambaye  amenusurika changamoto  ya  kumtoa  madarakani mwezi  Desemba , amedokeza  bungeni  jana  kwamba  angehitaji kuitisha  uchaguzi  mkuu  wa  taifa  kuweza  kupata  wingi kwa  ajili ya  kupitisha  sheria  ya  Brexit.

"Uwezekano  wa  bibi  May , kuazisha  uchaguzi  na  kuongoza  kundi la  wabunge  wa  chama  chake  cha  Conservative  kupata wabunge  wengi  watakaofikia  theluthi  ya  wabunge  wote  bungeni , ni ya  kichekesho," gazeti  la  Telegraph imewaambia  wasomaji wake.

Gazeti  lenye  wasomaji  wengi  nchini  Uingereza  la  The Sun , limemtaka  May  kujiuzulu  katika  taarifa  yake  ya  ukurasa  wa mbele  katika  toleo  lake  la  Jumatatu.

Gazeti  la  daily Mail , gazeti  jingine  ambalo linaunga  mkono  Brexit limeueleza  uamuzi  wa  bunge  kupiga  kura  dhidi  ya  mipango ya may  kuwa  ni "usaliti kwa Brexit" katika  ukurasa  wake  wa  mbele.

Brüssel Europäischer Rat | Donald Tusk, Statement zu Brexit
Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya Donald TuskPicha: Reuters/T. Melville

Katika  muda  wa  dakika  chache  baada  ya  bunge  kupiga  kura , hatua  iliyotokea  wakati  maelfu ya waungaji  mkono  Brexit wakifanya  maandamano  nje  ya  bunge , rais  wa  halmashauri  ya Umoja  wa  ulaya  Donald Tusk  alisema  viongozi  wa  Umoja  wa Ulaya  watakutana  Aprili  10  kujadili  kuondoka  kwa  Uingereza kutoka  kundi  hilo  la  mataifa.

Viongozi  kadhaa  wa  Ulaya  wamesema  kuna  nafasi  halisi kwamba  Uingereza  sasa  itajiondoa  bila  kupata  makubaliano, hali ambayo  makampuni  yanahofia  itasababisha  mtafaruku kwa uchumi  huo wa  tano  mkubwa  duniani.

Insert: Ripoti Kitojo

Mhariri: Iddi