1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uingereza, Rwanda kuwahamisha wahamiaji wiki chache zijazo

Tatu Karema
10 Aprili 2024

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak na Rais wa Rwanda Paul Kagame wamesisitiza kuwa wanatarajia kuwa wahamiaji wasio na vibali rasmi wataanza kupelekwa Rwanda kutoka Uingereza hivi karibuni.

https://p.dw.com/p/4edWN
 Rishi Sunak
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak Picha: Peter Morrison/AP Photo/picture alliance

Viongozi hao wawili wametilia mkazo hatua hiyo jana Jumanne mjini London, licha ya kuendelea kuibuka kwa maswali mapya kuhusu mpango huo tata.  

Msemaji wa serikali ya Uingereza amearifu kwamba Sunak amemfahamisha Rais Kagame kuhusu hatua zitakazofuata bungeni juu ya suala hilo lililoleta mvutano.

Kuwapeleka wahamiaji Rwanda, ni sehemu muhimu ya majibu ya Waziri Mkuu Sunak katika kukomesha kuingia kwa waomba hifadhi nchini Uingereza. 

UN yaitaka Uingereza kuachana na mpango wa kuwapeleka wahamiaji Rwanda

Wahamiaji hao huhatarisha maisha kwa kutumia usafiri wa boti ndogo wakitokea Ufaransa. Pendekezo la kuwaondoa wahamiaji Uingereza limekabiliwa na utata na changamoto za kisheria tangu aliyekuwa Waziri Mkuu Boris Johnson alipoliwasilisha mwaka 2022.