1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uitiwaji saini mkataba wa amani mashari ki ya Kongo waonekana kuchelewa

22 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cw7H

GOMA:

Mkataba wa amani kati ya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na makundi ya uasi mashariki mwa nchi hiyo unatarajiwa kutiwa saini katika sherehe mjini Goma.

Mkataba hu unahusu usitishwaji haraka wa mapigano,kuondoka kwa awamu kwa makundi yote ya waasi kutoka mkoa wa Kivu ya kaskazini na kuwarejesha makwao maelfu ya wananchi ambao wametoroka maeneo kutokna na mapigano. Wandishi habari wanasema kuwa majaliwa ya Generali muasi -Laurent

Nkunda, ambae anatakiwa kujibu makosa ya uhalifu wa kivita, hayakuhusishwa katika mkataba huo.Na hilo huenda ndilo jambo ambalo linonekana kama limesabaishwa kuchelewa kutia sahihi mkataba huo.Inasemekana kuwa waasi wamekataa kutia sahihi mktaba huo hadi suala hilo lipatiwe ufumbuzi.