1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani Chama cha Kijani chaadhimisha miaka 40

Zainab Aziz Mhariri: Sekione Kitojo
10 Januari 2020

Chama cha kijani cha walinzi wa mazingira kinaadhimisha mwaka wa 40 tangu kuanzishwa nchini Ujerumani. Hapo mwanzoni wanachama wake hawakutiliwa maanani na kuonekana kama mchanganyiko wa kundi la watu wasio na muelekeo.

https://p.dw.com/p/3W0Sh
Österreich Salzburg | Parteitag Die Grünen | Bildung Koalition mit ÖVP | Werner Kogler
Picha: Getty Images/AFP/APA/B. Gindl

Watu kutoka nasaba mbalimbali za kijamii walikutana katika mji wa Karlsruhe mnamo tarehe12 na13 mnamo mwaka wa1980. Vijana waliokuwa mahiri katika harakati za wanafunzi, mnamo mwaka1968 pia walihudhuria mkutano huo mjini Karlsruhe. Wengine walikuwa walinzi wa mazingira,wanaharakati wa kutetea amani, wahafidhina, walinzi wa wanyama, wakomunisti na wanaharakati wa kutetea haki za akina mama.

Akina baba wengi walikuwa na madevu na walivaa Jeans. Wanawake walivaa sweta za kufuma na mara nyingi walizifuma wenyewe. Baada ya mkutano huo wa mwaka 1980 chama cha kijani, kilianzishwa. Hata hivyo hapo mwanzoni chama hicho kilikuwa cha watu fulani tu. Hakikuwa wazi kwa wote.Vyama vikuu vya kisiasa nchini Ujerumani vilipigwa butaa. 

Tangu kumalizika vita vikuu vya pili ulingo wa siasa ulikuwa hodhi ya vyama vya CDU,CSU,SPD na FDP.

Hata hivyo mnamo mwaka 1983 chama cha kijani kilifanikiwa kuingia kwenye bunge la Ujerumani.Wakati huo wajumbe wa chama hicho walizingatiwa kama vioja na watukutu.

Muda mfupi baadae wajumbe wa chama hicho walianza kutumikia nyadhifa muhimu za kisiasa.Otto Schily aliyekuwa wakili wa mrengo wa shoto wa aliyekuwa mbunge mashuhuri Joschka Fischer ambaye hapo awali alikuwamo kwenye kundi la siasa kali la mrengo wa shoto katika jimbo la Hesse aliteuliwa kuwa waziri wa ulinzi wa mazingira. Mbunge wa chama cha kijani Michael Kellner ameiambia DW analiheshima sana rika hilo. Amesema watu hao wameleta mabadiliko makubwa nchini Ujerumani ndiyo sababu tunaona mafanikio katika chaguzi kutokana na kura za watu wenye umri wa miaka 60 na kwamba chama cha  kijani kinatambulika kwa harakati zakupinga nishati ya nyuklia na kuendesha harakati za kupinga mashindano ya silaha katika mashariki na magharibi.

Waziri wa zamani wa Mambo ya nje wa Ujerumani wa chama cha Kijani Joschka Fischer
Waziri wa zamani wa Mambo ya nje wa Ujerumani wa chama cha Kijani Joschka FischerPicha: picture-alliance/dpa/R. Vennenbernd

Masuala hayo  yalikuwamo katika ajenda ya chama cha Kijani. Miaka michache baadae Joschka Fischer aliteuliwa kuwa waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani. Chama cha kijani kiliongoza serikali kwa muda wa miaka saba pamoja na chama cha Social Demokratik.

Chama hicho kilianza kuyaona mabadiliko makubwa katika historia yake.Waziri Fischer aliunga mkono uamuzi wa kuwapeleka askari wa Ujerumai kushiriki katika juhudi za kuleta amani Kosovo na Montenegro bila ya idhini ya Umoja wa Mataifa. Hiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa wanajeshi wa Ujerumani kushiriki katika zoezi la kijeshi nje ya Ujerumani tangu kumalizika vita vikuu vya pili.

Kabla ya hapo Ujerumani ilikuwa inashiriki katika juhudi za kidiplomasia tu. Waziri Fischer alilaumiwa na wenzake na alitupiwa mfuko wa rangi. Hata hivyo kwa baadhi ya wanachama jambo muhimu lilikuwa misingi ya chama na sio sera za hapa na pale. Mabadiliko mengine yalitokea baada chama cha 90 Bündnis kutokea upande wa Mashariki kuungana na chama cha kijani. Muungano rasmi ulifanyika mnamo mwaka 1993. Mafanikio makubwa ya chama cha kijani yalipatikana mnamo mwaka 2002 ambapo hatua ya kwanza ya kuondokana na nishati ya nyuklia ilipigwa.

Mwenyekiti wa sasa wa chama cha Kijani Annalena Baerbock
Mwenyekiti wa sasa wa chama cha Kijani Annalena BaerbockPicha: picture-alliance/dpa/M. Kappeler

Tangu suala la ulinzi wa mazingira kuwamo katika ajenda za kila siku nchini Ujerumani chama cha kijani kimezidi kupata umaarufu hadi kufikia asilimia 20 na sasa chama hicho kimo katika serikali za majimbo 11 kati ya 16 ya nchini Ujerumani. Katika uchaguzi wa bunge la Ulaya, mwaka uliopita chama cha

Kijani kilifikia asilimia 20.5. Bwana Winfried Kretschmann ni mwanachama wa kwanza wa chama cha Kijani  kuwa waziri mkuu kwenye jimbo la Baden-Württemberg.

Vijana wengi wameejiunga na chama hicho na sasa chama hicho kimeongeza idadi ya wanachama kutoka 60,000 hadi 100000. Wachambuzi wanaamini kwamba chama cha Kijani kitakuwa na uwezekano mkubwa wa kuingia katika serikali kuu baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka ujao nchini Ujerumani.

Chanzo: Mwandishi DW/Thurau, Jens