1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani itasaidia utaratibu wa kidemokrasia Vietnam

1 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DGNC

HANOI:

Ujerumani ipo tayari kuisaidia Vietnam katika jitahada zake za kuanzisha mageuzi ya kidemokrasia.Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmeier wakati wa ziara yake mjini Hanoi,ametia saini makubaliano ya kusaidia kutoa mafunzo kwa majaji,wanasheria na watumishi wa serikalini nchini Vietnam.Steinmeier na waziri mwenzake wa Vietnam,Pham Gia Khiem wametia saini pia makubaliano ya kuanzisha chuo kikuu kipya katika mji wa Ho Chi Minh.Mradi huo wa pamoja utashughulikiwa na jimbo la Ujerumani la Hesse na Vietnam.