1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani kuandaa mkutano wa kimataifa kuwasaidia Wapalestina

15 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DOsS

BERLIN:

Serikali ya Ujerumani imesema itaandaa mkutano wa kimataifa utakaohusika na njia ya kuwasaidia Wapalestina katika sekta ya sheria na huduma za polisi kwa matayarisho ya taifa huru la Palestina.

Mbali na Wapalestina na Waisraeli,mkutano huo utahudhuriwa pia na Umoja wa Mataifa,nchi zote za Umoja wa Ulaya,idadi kadhaa ya nchi za Kiarabu,Marekani na Urusi.Mkutano huo utafanywa mjini Berlin mwanzoni mwa mwezi Juni.

Siku ya Ijumaa,Rais wa Wapalestina Mahmoud Abbas alipozungumza na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel kwa njia ya simu alisema anakaribisha hatua hiyo na akatoa mwito kwa Merkel kuishinikiza Israel kusitisha harakati za ujenzi wa makaazi mapya,atakapokwenda Israel siku ya Jumapili.