1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani kuitambua Kosovo

20 Februari 2008

Baraza la mawaziri la Ujerumani lakutana leo kuamua kuitambua nchi changa ya Kosovo.Urusi inakosoa utambuzi wa Kosovo.

https://p.dw.com/p/DAKf

Taarifa ya hivi punde kutoka Berlin, inasema serikali ya ujerumani inaidhinisha leo kuitambua Kosovo kama nchi huru.

Urusi imekosoa kwa ukali mno jibu la umoja wa ulaya la tangazo la uhuru.Na waziri wa nje Stephen Smith wa Australia amesema amehuzunishwa na uamuzi wa Serbia wa kumrejesha nyumbani balozi wake kwa kuwa Australia imeitambua Kosovo kuwa nchi huru.

Baraza la mawaziri la Ujerumani linakutana leo na kwa muujibu wa afisa mmoja wa serikali,Ujerumani ina azma ya kuiitambua jamhuri ya Kosovo.Tayari mapema wiki hii, waziri wan je wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier alitoa ishara hiyo kuwa Ujerumani itautautambua mkoa wa Kosovo uliopjitenga na Serbia kuwa ni nchi huru.

Kwa hatua hiyo, Ujerumani inajiunga na Marekani na wanachama wenzake wa umoja wa Ulaya kama vile Ufaransa na Uingereza kuitambua Kosovo kuwa ni dola huru.

Russia,China na baadhi ya wanachama wengine wa Umoja wa Ulaya kama Spain ,zimeupinga uamuzi wa kuitambua Kosovo.

Mkoa wa Kosovo uliojitangazia uhuru hapo jumapili,ukitawaliwa na Umoja wa mataifa tangu 1999.Licha yxa kugawika kwa wanachama 27 wa UU kuhusu kuitambua Kosovo nchi huru,zimeakubaliana kuimarisha ulinzi na usalama huko Kosovo.Zitatuma kikosi cha askari polisi 1,800 na ujumbe wa kisheria kuchukua nafasi ya Ujumbe wa sasa wa UM uliopo huko.

Russia,mshirika mkubwa wa Jamhuri ya Serbia imekosoa muitiko wa Umoja wa Ulaya wa Tangazo la uhuru la Kosovo .Wizara ya nje mjini Moscow, imearifu kwamba uamuzi wa UU kutuma kikosi cha askari 1.800 na Tume ya kisheria Kosovo ,hauna msingi wa kisheria na hivyo, utahitaji idhini ya Baraza la Usalama la UM.Ikaongeza Russia kusema kuwa kitendo cha UU kinahatarisha usalama barani ulaya na kinatilia shime majimbo mengine kujitenga ulimwenguni.

Tayari mshauri mkuu wa rais Mahmud Abbas wa Palestina, Abed Rabbo, amependekeza kwamba ikiwa majadiliano ya sasa na Israel yatashindwa,wapalestina wajitangazie uhuru wao.Akifuata hapo nyayo za Kosovo .

Athari za kujitangazia uhuru Kosovo zatazamiwa pia kuliathiri eneo la kaukasus , huko Asia ya kati:

Majimbo ya Abchasen na Osseten yanalililia pia uhuru wao.Pale Urusi iliposambaratika 1991,Abchasien ilidai kujitenga na kuwa huru kutoka Georgia.Rais wa wakati ule wa Georgia Eduard Schewartdnadse alituma haraka huko majeshi na kukandamiza kwa nguvu kilio cha uhuru.

Australia ni mojawapo ya dola kama Marekani, na Ujerumani zilizoitambua nchi changa ya Kosovo: Waziri wan je wa Australia, Stephen Smith ameelezea leo masikitiko kwa hatua ya Serbia ya kujibisha utambuzi huo kwa kumrejesha nyumbani nbalozi wake kutoka Canberra,Australia.

Smith akatumai kurejea nyumbani ijumaa hii ijayo kwa balozi Milivoje Glisic kutakua kwa muda tu na hakutadhuru usuhuba kati ya Australia na Serbia.Australia ilioitambua Kosovo kama dola jipya hapo jana ,imetangaza kwamba inatumai karibuni kuanzisha nayo uhusiano wa kibalozi.

Belgrade, imeamrisha kurudi nyumbani mabalozi wake kutoka Washington pamoja na miji mikuu ya nchi nyengine zilizoitambua nchi changa ya Kosovo.

Uturuki ni miongoni mwa nchi zilizoitambua Kosovo.