1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani kuumana na Norway; wahuni nje

Sekione Kitojo
4 Septemba 2017

Timu ya taifa  ya Ujerumani yawania kufuzu kucheza katika kombe la dunia nchini  Urusi mwakani, mazungumzo lakini  yakiwa mashabiki wahuni watakitakiwa kuzuiwa kuingia uwanjani mjini Stuttgart leo(04.09.2017).

https://p.dw.com/p/2jKx5
BG Confed Cup 2017 | Team Deutschland
Picha: picture alliance/dpa/C. Kolbert

Rais  wa   shirikisho  la  kandanda  nchini  Ujerumani  Reinhard Grindel  anataka  vyama  vya  kandanda  barani  Ulaya  kufanyakazi kwa  karibu  kupambana  na  tabia  mbaya  ya  wahuni  katika michezo  baada  ya  mashabiki  kuimba  kauli  mbiu  za  Wanazi katika  mchezo  wa  kufuzu  katika  fainali  za  kombe  la  dunia  mjini Prague ambapo  Ujerumani  ilikuwa  inacheza  dhidi  ya  Jamhuri  ya Cheki.

DFB Deutschland Training in Stuttgart Timo Werner
Mchezaji wa timu ya taifa ya Ujerumani Timo WernerPicha: picture-alliance/Pressefoto Rudel

Grindel  ameliambia  jarida  la  Kicker , kwamba " tunahitaji  kujadili suala  la  mauzo  ya  tikiti  kwa  pamoja  na  vyama  vya  kandanda barani Ulaya  na  kupata  njia  ya  kuhakikisha  udhibiti  zaidi  kote barani  Ulaya.

Grindel  alikosoa vikali  kundi  la  mashabiki  wapatao 200  wa Ujerumani  ambao  waliimba  kauli  mbiu za Wanazi  wakati  wa mchezo  huo  siku  ya  Ijumaa  ambapo  Ujerumani  iliishinda  kwa taabu Jamhuri  ya  Cheki  kwa  mabao 2-1. Pia  walimtusi mshambuliaji  wa  Ujerumani Timo Werner.

Kocha  wa  timu  ya  taifa  ya  Ujerumani Joachim Loew ameomba mashabiki  katika  mchezo  wa  leo  kati  ya  Ujerumani  na  Norway kuheshimu wachezaji  ambao  wamehama  kutoka  timu  zao kwenda kwingine kwasababu  huo  ni  uamuzi  wa  mtu  binafsi.

Fußball | Deutschland vs Nordirland | Jogi Löw
Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Joachim LoewPicha: picture-alliance/augenklick/S. El-Saqqa

Alikuwa akilenga  kuwatahadharisha  mashabiki  wa  Stuttgart  ambao huenda wakamuona  mshambuliaji  wa  timu  ya  taifa  ya  Ujerumani  Timo Werner  kuwa  ni  msaliti  baada  ya  mshambuliaji  huyo  kuimaha timu  hiyo  iliposhuka  daraja  na  kujiunga  na  RB Leipzig  ambapo hivi  sasa  anang'aa na timu  hiyo na  kuitwa  katika  ya  taifa.

Kundi C

Mchezo  mwingine  wa  kundi  C ni   kati  ya  Azerbaijan  dhidi  ya San Marino, na  Ireland  ya  kaskazini  inapambana  na  Jamhuri  ya Cheki.

Ubelgiji imekuwa  timu  ya  kwanza  katika  bara  la  Ulaya  kufuzu kucheza katika  fainali  za  kombe  la  dunia  mwakani  nchini  Urusi. Ushindi  wa  mabao  2-1  ugenini  dhidi  ya  Ugiriki  jana  Jumapili ulitosha  kuipeleka  timu  hiyo  katika  nafasi  ya  juu  katika  kundi  H na  kuingia  katika  fainali  yake  ya  pili  mfululizo  baada  ya kumaliza  katika  robo  fainali  katika  mashindano  ya  mwaka  2015 nchini  Brazil. Matokeo  ya  jana  yamerefusha  pia  rekodi  yake  ya timu  hiyo  kutoshinda  katika  michezo 11.

Fußball WM-Qualifikation Griechenland vs Belgien
Wachezaji wa Ubelgiji wakishangiria bao dhidi ya UgirikiPicha: Imago/Panoramic International

Italia iliyopata  jeraha  kwa  kipigo dhidi  ya  Uhispania  siku  ya Jumamosi  inataka  leo  kubadi  mkondo  wakati  itakapokuwa mwenyeji  wa  Israel  kesho  Jumaane  katika  mchezo  wa  kundi  G. Squadra  Azzuri  inahitaji  ushindi  ili  kujiimarisha  katika  nafasi  ya pili  katika  kundi  G  nyuma  ya  Uhispania  ili  kuwa  salama  dhidi ya  timu  inayoshikilia  nafasi  ya  tatu  Albania  wakati  wakijiweka vizuri  kufikia  fainali  nchini  Urusi mwakani.

Uhispania yafanya kweli

Nayo  Uhispania  iliyoifanyia  kitu  mbaya  Italia  kwa  kuicharaza mabao 3-0  siku  ya  Jumamosi inataka  kuimarisha  nafasi  yake kuwa  moja  kati  ya  timu zinazopigiwa  upatu  kunyakua  kombe  la dunia  mwakani  kwa  kutayarisha  kipigo  kingine  dhidi  ya Liechtestein kesho  Jumaane.

Nayo  Uholanzi  imeweka  matumaini  yake  hai  ya  kufikia  fainali  za mwakani  za  kombe  la  dunia  baada  ya  kuirarua Bulgaria  jana kwa  mabao 3-1 , lakini  Sweden iliikaanga  Belarus  kwa  mabao  4-0  na  kuifikia  Ufaransa  katika  msimamo  wa  kundi A jana  Jumapili kwa  kufikisha  pointi  16 .

Frankreich UEFA EURO 2016 Fußball EM Spanien - Türkei
Wachezaji wa Uhispania wakipongezana baada ya kufunga baoPicha: Reuters/Y. Herman

Kwa  nchi  tano  ambazo  bado  zinapambana  kuwania  nafasi  mbili za  moja  kwa  moja  kuingia  katika  fainali  za  mwakani  nchini Urusi , kampeni  ya  kufuzu  kuingia  katika  fainali  hizo  kwa  mataifa ya  Asia  imefikia  sasa  uamuzi  wa  dakika  90. Iran na  Japan tayari  zimefuzu  kuingia  katika  fainali  kama  washindi  wa  makundi A na  B, lakini  timu  hizo  mbili  bado  zinajukumu  la  kuamua  ni mahasimu  wao  gani , ikiwa  ni  mabingwa  wa  kombe  la  mataifa ya  Asia  , Australia   na  Korea  kusini , zitajiunga  nazo  katika fainali  za  kombe la  dunia  nchini  Urusi mwakani.

Timu  saba  za  Asia  zinaweza  kufuzu  ama  kwa  kumaliza  zikiwa nafasi  ya  pili  katika  makundi  yao  ama  kwa  kupitia  mchujo katika  bara  hilo  ama kutoka  bara moja  kwenda jingine.

Fußball Katar Mannschaft
Timu ya taifa ya Qatar ikifanya mazoweziPicha: Reuters/I. Al Omari

Iran inakuwa  mwenyeji  kwa  Syria inayowashangaza  wengi , timu ambayo  haikuweza  kucheza  nyumbani  kutoka  na  hali  ya  kivita nchini  humo, lakini  imejisogeza  hadi  nafasi  ya  tatu  katika  kundi A wiki  iliyopita  kwa  ushindi  wa  mabao 3-1  dhidi  ya  Qatar. Licha ya  kushindwa  kujitayarisha  kwa  njia  ya  utulivu , Syria  bado  ina nafasi  ya  kufuzu kucheza  katika  fainali  yake  ya  kwanza  ya kombe  la  dunia  iwapo  matokeo  yatakuwa  mazuri kesho Jumanne.

Syria  lakini  inalazimika  kushinda  mjini  Tehran   na  kutegemea Korea  kusini ipoteze  mchezo wake kwa ushindi  mdogo dhidi  ya Uzbekistan.

 

Mwandishi: Sekione  Kitojo / afpe / dpae / rtre

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman