1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani na Austria zatishiwa kushambuliwa

21 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CPlq

Ukanda mpya wa video wa watuhumiwa wanamgambo wa itikadi kali za Kiislam umetolewa kwenye mtandao ukitishia kufanya mashambulizi dhidi ya Ujerumani na Austria iwapo nchi hizo hazioondowa wanajeshi wao kutoka Afghanistan.

Ukanda huo umeonyeshwa na televisheni ya Austria hapo jana jioni.Wanamgambo hao wamejitambulisha kuwa the Global Islamist Media Front.

Ujerumani ina wanajeshi 3,000 waliowekwa nchini Afghanistan ikiwa ni sehemu ya kikosi cha Kimataifa cha Usaidizi wa Usalama ISAF kinachoongozwa na Jumuiya ya Kujihami ya Mataifa ya Magharibi NATO.

Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Wolfgang Schäuble amesema serikali inaungalia ukanda huo kwa makini lakini Ujerumani haigopeshwi na vitisho