1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani na Ulaya kusaidia kuimarisha usalama Afrika

Amina Mjahid
1 Novemba 2023

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, amesema taifa lake pamoja na Umoja wa Ulaya zimejitolea kuimarisha usalama Afrika Magharibi, na wanaweza kutoa mafunzo na vifaa ili kuunga mkono operesheni dhidi ya uasi.

https://p.dw.com/p/4YHBi
Scholz na Nana Akufo-Addo
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz na Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo Picha: picture alliance/dpa

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, amesema taifa lake pamoja na Umoja wa Ulaya zimejitolea kuimarisha usalama Afrika Magharibi, na wanaweza kutoa mafunzo na vifaa ili kuunga mkono operesheni dhidi ya uasi- unaosambaa katika eneo hilo.

Akizungumza nchini Ghana hapo jana, Scholz alisema kuenea kwa mapinduzi katika mataifa ya Afrika Magharibi, kumesimamisha ushirikiano wa nchi kwa nchi na huenda wanamgambo wakachukua nafasi hiyo kujiimarisha.

Ziara ya Scholz Nigeria: Ujerumani kufanya biashara ya nishati na Nigeria

Afrika Magharibi, inapambana na uasi ulioanza nchini Mali mwaka 2012 na kusambaa katika eneo zima la Sahel, kusini mwa Sahara na kusababisha mauaji ya maelfu ya watu na kuwaacha zaidi ya watu milioni 6 bila makaazi.

Scholz amesisitiza umuhimu wa kurejesha utawala wa kidemokrasia na kusema kwamba Ghana ni taifa la matumaini kwa eneo zima na mshirika wa karibu wa Ujerumani.