1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yaadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa demokrasia

Zainab Aziz
19 Januari 2019

Ujerumani leo inaadhimisha mwaka wa 100 tangu kuanzishwa demokrasia baada ya bunge kupitisha katiba ya kisasa katika mji wa mashariki wa Weimar mnamo mwaka 1919.

https://p.dw.com/p/3BpHR
Deutschland Frauenwahlrecht
Picha: picture-alliance/AdsD/Friedrich-Ebert-Stiftung

Wajerumani walipiga kura hata katika enzi ya ufalme lakini ukweli ni kwamba siyo wote waliokuwa na haki hiyo. Baada ya utawala wa kifalme kuangushwa bunge ndilo lililokuwa mhimili wa mamlaka na lilipitisha katiba ya kisasa lakini alikuwapo adui mkubwa wakati huo, Adolf Hitler. 

"Kila kitu ni kwa ajili ya umma na kitafanywa na umma". Hayo ni maneno aliyotamka kiongozi wa chama  cha Demokratik, SPD bwana Philpp Sheidemann kutokea kwenye roshani ya bunge mnamo mwaka 1918. Bwana Scheidemann aliitangaza Jamhuri siku hiyo iliyokuwa ya muda lakini wananchi waliruhusiwa kupiga kura miezi miwili baadae yaani siku kama ya leo miaka 100  liyopita.

Wakati huo palikuwa na baraza la mpito ndilo lilikuwa linaongoza serikali chini ya uongozi wa mwenyekiti wa chama cha SPD Friedrich Ebert. Jukumu lake lilikuwa kuiongoza serikali ya mpito baada ya utawala wa mfalme kuangushwa na kuipeleka nchi kwenye njia ya utawala wa demokrasia ya bunge.

Lakini maalfu ya watu walikufa katika njia hiyo kutokana na hali iliyokaribia vita vya wenyewe kwa wenyewe vya nchini Ujerumani. Miongoni mwa waliokufa alikuwa Rosa Luxembourg na Karl Liebknecht walioanzisha chama cha kikomunisti katika mwaka mpya. Wakomunisti hao mwashuhuri waliuliwa siku nne kabla ya kufanyika kikao cha bunge la katiba. Mauaji hayo hayakuwa nyota njema kwa kuzaliwa demokrasia nchini  Ujerumani.

Mnamo mwezi wa Desemba mwaka 1918 bunge la Ujerumani lililokuwa linadhibitwa na wademokrats  liliamua kujiengua lenyewe na hivyo kutoa fursa ya kupigwa kura ya haki na ya siri kwa mara ya kwanza  katika historia ya Ujerumani.

Na kwa mara ya kwanza wanawake pia waliruhusiwa kushiriki katika kupiga kura au kusimama katika  chaguzi. Hatua nyingine muhimu iliyochukuliwa ilikuwa ni kupunguza umri wa kuruhusu kupiga kura kutoka  miaka 25 hadi 20.

Lakini matumaini ya chama wademokrats ya kupata kura za kutosha kuunda serikali peke yao  haukutimia.  Chama hicho kilipata asilimia 37.9 ya kura. Kiwango hicho hakikutosheleza kuunda serikali, chama hicho kilipaswa kushirikiana na wahafidhina, wakatoliki na chama cha mrengo wa shoto wa wastani DDP.

Berlin barabara ya Alexanderplatz mnamo mwaka 1919
Berlin barabara ya Alexanderplatz mnamo mwaka 1919Picha: picture-alliance/akg-images

Chama cha kikomunisti hakikushiriki katika uchaguzi kwa sababu ingelimaanisha kuyasaliti mapinduzi. Kiongozi mashuhuri wa chama hicho Rosa Luxembourg aliwashauri wenzake kutoususia uchaguzi. Mwanasiasa huyo  alitambua kuwa chama cha SPD kilikuwa na nguvu kubwa zaidi miongoni mwa tabaka la wafanyakazi.

Kutokana na chama cha kikomunsiti  kujiweka kando ya uchaguzi, wasocial democrats na chama huru cha USPD walinufaika. Chama cha SPD kilishinda katika takriban sehemu zote. Mtaalamu wa historia Marcel Bois amesema sehemu kubwa ya Ujerumani ilikuwa ni rangi nyekundu wasocial demokrats walishinda takriban kwenye maeneo yote ya uchaguzi. Pia katika eneo la viwanda la Halle-Merseburg, chama cha USPD kilishinda na upande wa mashariki, kuna maeneo ambayo chama cha DNVP kilichopambana na chuki dhidi ya wayahudi kilikuwa na nguvu zaidi.

Wiki mbili baada ya uchaguzi bunge la taifa lilikutana kwa mara ya kwanza, siyo mjini Berlin bali katika mji wa Weimar. Yalifuatia matukio muhimu baada ya kikao cha bunge hilo. Mnamo mwaka 1920 Adolf Hitler alianzisha chama chake cha NSDAP kilipata nguvu miaka 10 baadae kutokana na mgogoro wa kiuchumi. 

Hatua nyingine muhimu ni kugawanya mamlaka katika mihimili ya Bunge, dola na mahakama ambapo mpaka leo Ujerumani inaongozwa katika msingi huo ila tu mamlaka ya rais sasa yamebakia kuwa ya uwakilishi tu na siyo ya utendaji tangu mwaka 1949. 

Mwandishi:Zainab Aziz/Fürstenau, Marcel/ LINK:

Mhariri:Yusuf Saumu