1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yaahidi kupeleka misaada nchini Libya

Lilian Mtono
14 Septemba 2023

Jeshi la anga la Ujerumani linajiandaa kupeleka misaada ya kiutu katika eneo lililoathiriwa na mafuriko mashariki mwa Libya.

https://p.dw.com/p/4WKsz
Moja ya ndege ya mizigo ya jeshi la Ujerumani- Bundeswehr
Moja ya ndege ya mizigo ya jeshi la Ujerumani- BundeswehrPicha: Hauke-Christian Dittrich/AFP/Getty Images

Jeshi la anga la Ujerumani linajiandaa kupeleka misaada ya kiutu katika eneo lililoathiriwa na mafuriko mashariki mwa Libya.

Ndege mbili za mizigo zinatarajiwa kuondoka katika kambi ya kijeshi ya Wunstorf ikiwa na misaada ambayo ni pamoja na magodoro, mahema, mablanketi, vitanda na majenereta.

Soma pia:Juhudi za kuisadia Libya zashika kasi

Ujerumani imeahidi kupeleka misaada hiyo mara moja baada ya Libya kuuomba Umoja wa Ulaya kuisaidia. 

Kimbunga Daniel kiliipiga Libya, ambayo tayari imeathirika na vita siku ya Jumapili na kulingana na serikali idadi ya vifo huenda ikafikia watu 20,000.