1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yatoa msaada zaidi kupambana na janga la njaa

Martin,Prema/ZPR8 Agosti 2011

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Guido Westerwelle ametangaza msaada zaidi kupambana na janga la njaa katika Afrika ya Mashariki.

https://p.dw.com/p/Redz
German Foreign Minister Guido Westerwelle speaks during a joint press conference with his Afghan counterpart Zalmai Rasool, not pictured, at the foreign ministry in Kabul, Afghanistan on Thursday, July 21, 2011. Westerwelle is on an official visit to Kabul to discuss issues of mutual interest and regional security. (Foto:Musadeq Sadeq/AP/dapd)
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Guido WesterwellePicha: dapd

Westerwelle, amesema, serikali ya Ujerumani itaimarisha msaada wake ili kurahisisha maisha ya wakimbizi, na hasa wanaotokea Somalia. Akaongezea, hivi karibuni pia, mjumbe maalum wa masuala ya Afrika katika wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani, Walter Lindner, atafanya ziara nchini Tanzania, Uganda na Kenya. Nchini Kenya atatembelea pia kambi ya wakimbizi ya Dadaab, iliyo kubwa kabisa duniani.

ARCHIV - Somalische Flüchtlinge am 08.07.2011 im Camp Dagahaley im kenianischen Dadaab in Afrika. Sie werden vom Welternährungsprogramm (WFP) mit Lebensmitteln und vom UNHCR mit Gegenständen des täglichen Bedarfs versorgt. Die Vereinten Nationen haben die kenianische Regierung dringend dazu aufgerufen, ein weiteres Flüchtlingscamp für die von der Dürre am Horn von Afrika betroffenen Menschen zu eröffnen. Foto: WFP/Rose Ogola (zu dpa0153 vom 12.07.2011 - ACHTUNG: Nur zur redaktionellen Verwendung bei vollständiger Quelle «WFP/Rose Ogola») +++(c) dpa - Bildfunk+++ pixel
Wakimbizi wa Kisomali katika kambi ya DadaabPicha: Picture-Alliance/dpa

Wakati huo huo, shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi-UNHCR- limesema kuwa leo ndege itapeleka msaada wa dharura mji mkuu wa Somalia Mogadishu. Hii ni mara ya kwanza tangu miaka mitano, kwa UNHCR kufanya operesheni kama hiyo.

Kwa mujibu wa shirika hilo, katika kipindi cha miezi miwili iliyopita, hadi Wasomali 100,000 wamekimbilia Mogadishu kutafuta chakula, maji na makaazi. Umoja wa Mataifa umesema, zaidi ya watu milioni12 katika Pembe ya Afrika wanahitaji msaada wa dharura kwa sababu ya ukame mbaya kabisa kutokea, tangu miongo kadhaa.

Inatathminiwa kuwa katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita, zaidi ya watoto 29,000 waliokuwa chini ya umri wa miaka mitano wamefariki kwa sababu ya njaa na ukame katika Pembe ya Afrika.