1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yaunga mkono Nigeria kuwa kwenye G20

Bruce Amani
31 Oktoba 2023

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz ameelezea kuiunga mkono Nigeria kukubaliwa katika kundi la madola yenye nguvu kiuchumi duniani la G20.

https://p.dw.com/p/4YEtb
Kansela Olaf Scholz (kulia) akizungumza na waandishi wa habari mjini Abuja akiwa na mwenyeji wake, Rais Bola Tinubu wa Nigeria.
Kansela Olaf Scholz (kulia) akizungumza na waandishi wa habari mjini Abuja akiwa na mwenyeji wake, Rais Bola Tinubu wa Nigeria.Picha: Kola Sulaimon/AFP/Getty Images

Akizungumza akiwa ziarani Lagos, Scholz amesema ukweli kwamba nchi kubwa kama Nigeria, ambayo ndiyo kubwa zaidi kiuchumi barani Afrika, inadai kuwa sehemu ya kundi hilo, ni sahihi.

Kansela huyo wa Ujerumani ameongeza kuwa kukubaliwa kwa Umoja wa Afrika - AU katika kundi hilo kunaashiria mafanikio, lakini hiyo haitoshi.

Soma zaidi: Ujerumani kufanya biashara ya nishati na Nigeria

Aidha, alibainisha kuwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa halina wawakilishi wa kudumu kutoka Afrika au Amerika Kusini.

Ujerumani kwa muda mrefu imekuwa ikishinikiza mageuzi ya chombo muhimu cha Umoja wa Mataifa.

Awali, Scholz aliielezea Nigeria kuwa mshirika muhimu kwa Ujerumanikatika uzalishaji wa gesi ya haidrojeni na kisha ununuzi wa gesi asilia.