1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makaidi wa NLD hayuko nasi tena

Sudi Mnette15 Oktoba 2015

Mwenyekiti wa chama cha National League for Democracy na pia mwenyekiti mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi Tanzania (UKAWA), Emanuel Makaidi, amefariki dunia akitibiwa mkoani Lindi kusini mwa nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/1Goyc
Ringen um neue Verfassung in Tansania
Picha: DW/M.Khelef

NLD ni mojawapo ya vyama vinne vya upinzani vinavyounda muungano wa UKAWA, ambao umemsimamisha mgombea mmoja wa urais katika uchaguzi wa Oktoba 25. Makaidi, aliyejizolea umaarufu kwenye umoja huo wa upinzani kama mwanadiplomasia na msuluhishi wa migogoro, alifariki dunia kwa ugonjwa wa moyo. Sudi Mnette anazungumza na mratibu wa shughuli za UKAWA, Dk. George Kahangwa, ambaye anathibitisha kifo hicho.

Mwandishi: Sudi Mnette
Mhariri:Yusuf Saumu

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi

Gundua zaidi