1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukosefu wa Maji Nchini Tanzania wawanufaisha wafanyabiashara wa maji ya mikokoteni.

Scholastica Mazula28 Mei 2008

Takribani asilimia ishirini na tano ya wakaazi milioni nne wanaoishi jijini Dare es Salaam, nchini Tanzania wana mambomba ya maji majumbani mwao.

https://p.dw.com/p/E7kj
Wananchi wa Japan wakijaza maji kwa ajili ya matumizi yao.Picha: AP

Hata hivyo mambomba mengi yamekuwa hayatoi maji ya kuweza kuwatosheleza watu wote.

Hii ni kwa mujibu wa Mamlaka ya maji safi na maji taka ya Mjini Dar es Salaam-DAWASCO.

Katika maeneo ya watu masikini ambao hawana kabisa mambomba wanategemea zaidi maji ya kununua kutoka kwa wauzaji wanaotembeza mitaani.

Juma Membe ni mfanyabiashara anayepita kila mlango akiuza maji katika mitaa ya watu masikini jijini Dar es Salaam na mara zote mkokoteni wake huonekana umejaa mapipa ya maji na wala hakuna anayekataa kuyauza kutokana na uhaba wa mambomba ya maji.

Juma Membe anasema hii ni biashara nzuri sana kwa sababu watu kila siku wanatumia maji.

Hata hivyo Meneja uhusiano wa Shirika la Maji safi na Maji Taka katika jiji la Dar es salaam na maeneo mengine ya pwani, Badra masoud, anasema si wauzaji wote wa maji wanaouza maji safi na salama.

Anafafanua kwamba ukosefu wa ajira umewafanya watu kutafuta njia mbalimbali za kujiingizia kipato, hivyo huuza maji tu pasipo kuzingatia usalama wake wanachozingatia wao ni fedha.

Hata hivyo kuna baadhi ya maeneo ambayo kuna mambomba ya maji lakini hayatoi maji, DAWASCO, kwa kushirikiana naa Serikali wanalishughulikia tatizo hilo na wamekuwa wakifanya miradi mbalimbali ili kuhakikisha watu wote wanapata huduma ya maji bila matatizo.

Aidha kumekuwa na malalamiko ya wananchi kuwa wamekuwa wakipewa gharama ya maji pasipo wao kupata huduma hiyo, Badra Masoud anakubali kuwa tatizo hilo lipo na Dawasco inatoa wito kwa watu wanapata matatizo hayo kutoa taarifa mapema ili kuepusha hali hiyo.

Anasema kuna Mpango waliouanzisha wa vioski vya maji mbao umeweza kuwanufaisha wakaazi wengi wa jiji hilo kama anavyothibitisha Havijawa Shabani alipozungumza na Shirika la Habari la IPS.

Havijawa ni msimamizi wa Kiosiki kimoja kilicho kando ya barabara, anasema amekuwa akipata wateja wengi kituoni hapo kutokana na eneo hilo kwanza kuwa karibu na makazi yao na pili kutokana na gharama za maji kuwa ndogo.

Mshauri wa masuala ya misaada ya maji nchini Tanzania Ben Taylor, anasema kwa makadilio ya matumizi ya kawaida ya maji kwa siku, kwa ajili ya kupikia, kunywa na usafi ni kama lita ishirini kwa mtu mmoja.

Anasema hii inamaanisha kwa kwamba familia ya watu watano inaweza kutumia gharama nyingi zaidi kwenye maji kwa siku.

Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2004, zilizotolewa katika ripoti ya pamoja kwa ushirikiano wa mpango wa usambazaji na usafishaji majim, Shirika la Afya duniani pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, idadi ya watanzania wanaopata huduma ya maji safi na salama inafikia asilimia siti.