1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine yataka ifunguliwe njia za bidhaa zake kwa Poland

Sudi Mnette
23 Novemba 2023

Ukraine imetaka njia inazotumia kusafirisha bidhaa zake kupitia Poland zifunguliwe kabla ya kukaa kwenye mazungumzo na serikali ya mjini Warsaw.

https://p.dw.com/p/4ZN0Y
Polen LKW Fahrer blockieren Grenzübergang zu Ukraine
Madereva wa maloli wa Poland wakiwazuia wenzao wa Ukraine katika eneo la mpaka la DorohuskPicha: Omar Marques/AA/picture alliance

Kauli hiyo inatolewa pamoja na halmashauri ya Umoja wa Ulaya, yanayolenga  kumaliza mgomo unaofanywa na madereva wa Malori wa Poland. Mgomo huo umechochea kupungua kwa shughuli za kibiashara za Ukraine. Madereva wawili wa Ukraine wamekufa na maelfu ya malori yamekwama kwa siku kadhaa, katika baridi kali,huku madereva wa malori wa Poland wakizifunga barabara,  za kuelekea kwenye vivuko vitatu katika mpaka kati ya nchi yao na Ukraine,ambayo ni njia muhimu kwa biashara za Ukraine wakati huu wa uvamizi wa Urusi.Madereva wa Poland walianza kuzifunga njia tangu Novemba 6 kupinga kile wanachosema ni kupokonywa biashara na madereva wa Ukraine ambao hawalazimiki kutafuta kibali cha kuvuka mpaka wa Poland tangu nchi yao ilipovamiwa na Urusi.