1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine kuweka eneo la usalama kwa raia

11 Juni 2014

Rais mpya wa Ukraine Poroshenko amewaamuru maafisa wa usalama kuweka eneo salama ili kuwawezesha raia kupita kutoka majimbo ya mashariki yaliyokumbwa na mapigano dhidi ya wanaotaka kujitenga wanaoiunga mkono Urusi.

https://p.dw.com/p/1CFTv
Ukraine Präsident Petro Poroschenko Vereidigung 07.06.2014 Player-Version
Rais Petro Poroshenko wa UkrainePicha: Reuters

Katika taarifa iliyochapishwa mtandaoni, Petro Poroshenko ameamuru vyombo vya usalama kutayarisha usafiri pamoja na maeneo kuwasaidia raia waweze kuondoka kutoka katika maeneo yaliyoathirika. Taarifa fupi ya Poroshenko haikutoa taarifa zaidi juu ya raia hao watapelekwa sehemu gani, ama ni makaazi ya aina gani wametaarishiwa.

Poroshenko pia ametangaza kuteuliwa kwa mkuu wa vyombo vya habari na mshirika wake katika masuala ya biashara Boris Lozhkin kuwa mnadhimu mkuu na Svyatoslav Tsegolka , ambaye ni mwandishi habari katika kituo cha televisheni kinachomilikiwa na Poroshenko , kuwa mwandishi wake mkuu wa habari.

Lawrow PK in Moskau 12.05.2014
Waziri wa Mambo ya kigeni wa Urusi Sergei LavrovPicha: Yuri Kadobnov/AFP/Getty Images

Jeshi halifanyiwa mabadiliko

Rais huyo mpya hakutangaza mabadiliko yoyote katika jeshi ama wizara ya mambo ya kigeni, ambako mabadiliko yangekuwa muhimu kwa mashambulizi yanayoendelea nchini Ukraine upande wa mashariki.

Hatua za Poroshenko kuunda eneo salama kwa ajili kupita raia inakuja wakati kuna hofu inayoongezeka kuwa kampeni kubwa ya serikali dhidi ya waasi imechangia ongezeko kubwa la vifo vya raia upande wa mashariki.

Maafisa wa serikali wanasema kiasi ya watu 200 , ikiwa ni pamoja na wanajeshi 59, wameuwawa katika mashambulizi upande wa mashariki.

Anti-Kriegs-Demo Ukraine
Majeshi ya serikali UkrainePicha: Reuters

Urusi yakaribisha hatua ya Ukraine

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi UNHCR limesema mwezi Mei kuwa hali ya wasi wasi nchini Ukraine imesababisha kiasi ya watu 10,000 kukimbia makaazi yao, kutoka jimbo lililochukuliwa na Urusi la Crimea na kutokana na ghasia upande wa mashariki, lakini kabla ya tangazo la leo hakuna msaada rasmi wa serikali uliotangazwa kwa ajili ya watu wa mashariki.

Taarifa ya Poroshenko inatoa ishara kuwa anapanga kumaliza operesheni za serikali dhidi ya waasi, ambao wameendelea kushikilia majengo ya serikali, vituo vya polisi, vituo vya mpakani na makambi ya jeshi katika eneo hilo.

Wakati huo huo Urusi imesema leo kuwa inakaribisha uamuzi wa Ukraine wa kuweka eneo salama katika upande wa mashariki lakini imesisitiza kuwa Urusi bado haioni kupungua kwa mzozo wa Ukraine.

Steinmeier mit Lawrow und Sikorski 10.06.2014 in St. Petersburg
SteinmeirShoto) , Lavrov(kulia) na Sirkorski (Kati) wakikutanaPicha: picture-alliance/dpa

Hayo yamesemwa na waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi Sergei Lavrov baada ya mazungumzo na waziri mwenzake wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier pamoja na waziri wa mambo ya kigeni wa Poland.

Waziri Steinmeier amesema katika mazungumzo hayo kuwa pande zote zinaonekana kuwa zina nia ya dhati kupunguza mzozo huo kufuatia siku tatu za mazungumzo yao.

Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe

Mhariri : Mohammed Abdul Rahman