1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine yadai kuishambulia meli kuu ya kijeshi ya Urusi

14 Aprili 2022

Ukraine imedai leo kuwa iliishambulia meli kuu ya Urusi katika bahari Nyeusi kwa makombora, na kusababisha moto ambao Moscow imesema umeiharibu vibaya meli hiyo muhimu ya kivita

https://p.dw.com/p/49xYU
Russland Kreuzer Moskva
Picha: Alexey Pavlishak/REUTERS

 Meli hiyo ya Moskva ambayo ilitumiwa awali katika mozozo wa Syria, ndiyo ilikuwa inaongoza mashambulizi ya majini ya jeshi la Urusi dhidi ya maeneo ya pwani na ndani ya kusini mwa Ukraine, katika vita vyake vya uvamizi vilivyodumu kwa karibu wiki saba sasa.

Vyombo vya habari vya serikali ya Urusi havikutaja chochote kuhusu shambulio la kombora vilipoinukuu wizara ya ulinzi ikisema kwamba zana ziliripuka ndani ya meli ya Moskva na kusababisha moto ulioiharibu vibaya meli hiyo, na kuongeza kuwa mabahari wake walikuwa wameondolewa.

Maafisa wawili kutoka Odessa, ambao ni mji muhimu wa bandari wa Ukraine kwa biashara na ulinzi, walithibitisha kuwa vikosi vya Ukraine viliishambulia meli hiyo.

Somazaidi:Urusi yalaumiwa kwa ukiukaji wa sheria za kimataifa za kibinadamu nchini Ukraine.

Maafisa hao waliongeza kuwa adui yao alipoteza wanajeshi 54 katika shambulio hilo, ambalo meli hiyo inayojulikana kama Moskva ilipigwa na kombora la kushambulia meli la Neptune katika eneo la operesheni la bahari Nyeusi.

"Meli hiyo inayoongoza operesheni za urusi katika bahari Nyuesi ilipata uharibifu mkubwa" alisema Vladislav Nazarov, kutoka kamandi ya kusini ya jeshi la Ikraine.

 Lisisitiza kwamba moto ulianza na vintego vingine vya kikosi cha majini vilijaribu kutoa msaada, lakini dhoruba na mripuko mkubwa wa silaha uliipindua meli hiyo na ikaanza kuzama.

Urusi: Moto haukuharibu mfumo wa kurusha makombora

Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema moto huo ulizimwa na meli hiyo imebaki ikielea na kwamba mfumo wake mkuu wa kurusha makombora haukuharibiwa.

Russland | Präsident Putin im russischen Weltraumbahnhof Kosmodrom Wostotschny
Rais wa Urusi Vladimir PutinPicha: Evgeny Biyatov/Kremlin/Sputnik/REUTERS

Moto katika meli hiyo kuu ulitokea saa chache baada ya Marekani kutangaza ufadhili mpya wa dola milioni 800 kwa Ukraine, ambao unahusisha ununuzi wa zana nzito za kivita, makhsusi kwa ajili ya mashambulizi makubwa yanayotarajiwa ya ardhini, ikiwemo ndege, magari ya kivita na helikopta.

Soma zaidi:Umoja wa Ulaya kuisaidia Ukraine kujiunga na Umoja huo

Meli za Urusi katika bahari Nyeusi zimekuwa zikiuzingira mji wa Mariupol, ambako jana Jumatano, wizara ya ulinzi ya Urusi ilisema wanajeshi wake wamechukuwa udhibiti kamili wa banadari.

Ilitangaza kuwa zaidi ya wanajeshi 1,000 wa Ukraine mjini Mariupol wamejisalimisha, huku mashambulizi ya anga yakilenga kiwanda kikubwa cha chuma cha Azovstal, madai ambayo Ukraine imeyakanusha.

Oparesheni ya kijeshi ya urusi, Ukraine imekwenda kama ilivyopangwa?

Awali kutarajia kumshinda jirani yake kwa haraka, Urusi imekabiliwa na upinzani mkali nchini Ukraine na sasa inakabiliwa na mashambulizi ya kisasi katika ardhi yake.

Wa-Ukraine waapa kutetea maeneo yao

Siku ya Jumatano moscow ilitangaza kutishia kushambulia maeneo ambako maamuzi yanafanyika nchini Ukraine, ikiwemo mji wa Kyiv, endapo Kyiv itaendeleza mashambulizi katika ardhi ya Urusi.

Soma zaidi:Njia zaidi za kiutu zaundwa Ukraine

Wakati mapigano hayo yakiendelea shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR, limeripoti leo kwamba raia milioni 4.7 wa Ukraine wameikimbia nchi hiyo katika siku 50 za uvamizi wa Urusi.

Shirika hilo limeutaja mzozo huo wa wakimbiziunaoendelea kushuhudiwa kukua kwa kasi katika mataifa ya Ulaya,ni mkubwa zaidi barani humo tangu vita kuu ya pili ya dunia.

Chanzo:Mashirika