1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukuaji uchumi kanda ya euro wakwama

14 Agosti 2014

Ukuaji wa uchumi wa mataifa ya kanda ya euro umekwama bila kutarajiwa katika robo ya pili ya mwaka huu ukivutwa chini kutokana na kunywea kwa uchumi wa Ujerumani pamoja na Ufaransa ambayo uchumi wake umekwama.

https://p.dw.com/p/1Cuea
EZB billiges Geld Symbolbild
Nembo ya euroPicha: picture-alliance/dpa

Hali hiyo inayotoa ishara ya hatari kuhusiana na uchumi wa kanda ya sarafu ya euro ambayo inapitia kipindi cha kupambana na athari za vikwazo dhidi ya Urusi.

Uchumi wa nchi 18 za kanda ya euro haukuweza kukua katika miezi mitatu hadi Juni mwaka huu ikilinganishwa na robo ya kwanza ambapo ukuaji ulifikia asilimia 0.2.

Ujerumani ambayo ina uchumi mkubwa katika bara la Ulaya umenywea kwa asilimia 0.2 katika robo ya kwanza ya mwaka huu, kinyume na makadirio ya benki kuu ya Ujerumani , Bundesbank, kwamba uchumi huo hautaongezeka, wakati biashara ya nje na uwekezaji zikiwa ni sehemu zilizoonesha udhaifu mkubwa , imeeleza ofisi ya takwimu leo Alhamis.

Italiens Premier Matteo Renzi im Europoäischen Parlament 02.07.2014
Waziri mkuu wa Italia Matteo RenziPicha: Reuters

Kutokana na hali ambayo haina uhakika inayotokana na mzozo kati ya Urusi na Ukraine , kurejea kwa haraka kwa mafanikio hakutarajiwi.

Ufaransa iko katika hali bora kidogo

Ufaransa ilikuwa bora kidogo , ikiwa na kiwango kile kile cha ukuaji kwa robo ya pili mfululizo.

Hali hiyo imeilazimisha serikali ya Ufaransa kuikabili hali halisi, ikisema itashindwa kufikia lengo lake la nakisi katika bajeti kwa mara nyingine mwaka huu na kupunguza makadirio yake ya ukuaji wa uchumi kwa mwaka 2014 kwa moja asilimia katika nusu ya kwanza ya mwaka.

Tarakimu za pato jumla kwa ajili ya eneo la sarafu ya euro kwa jumla zitapatikana baadaye leo na utabiri unaonesha ukuaji mdogo wa asilimia 0.1.

Kutokana na ripoti kutoka mataifa wanachama tayari zimekwisha wasili , hata lengo hilo huenda likashindikana kufikiwa.

Mario Draghi EZB Sitzung am 03.07.2014
Mkuu wa benki kuu ya Ulaya Mario DraghiPicha: Reuters

Data katika wiki chache zilizopita zimeonesha hapo kabla Uhispania ambayo ilikuwa katika hali mbaya , imepata ukuaji wa asilimia 0.6, kasi ambayo hakuna moja kati ya nchi zingine inaweza kuivuka.

Italia, ikiwa na uchumi wa tatu kwa ukubwa katika kanda ya euro , imetumbukia katika mdororo wa uchumi kwa mara ya tatu tangu mwaka 2008 katika robo ya pili, uchumi wake ukinywea kwa asilimia 0.2 na kumshinikiza waziri mkuu Matteo Renzi kufanya mageuzi makubwa ya bajeti aliyoyaahidi.

Italia na Ufaransa zimeongoza juhudi za kulenga sera za Umoja wa Ulaya kuhusiana na ajira na ukuaji badala ya kupunguza madeni.

Ujerumani na mataifa mengine yameonesha kwamba yatavumilia tu mjadala huo hadi wakati fulani.

Sarafu ya euro yapaswa kuimarishwa

Mkuu wa benki kuu ya Ujerumani Jens Weidmann amesema jana kuwa sera ya kifedha ya kanda ya euro haipaswi kulenga kudhoofisha sarafu ya euro pamoja na mataifa wanachama yanapaswa kuchukua hatua kuimarisha ukuaji wa uchumi, akipuuzia miito ya Ufaransa kwa Ujerumani na benki kuu ya Ulaya kuchukua hatua zaidi.

EZB frankfurt nacht main
Makao makuu ya benki ya Ujerumani mjini FrankfurtPicha: dpa

Ukusanyaji wa maoni uliofanywa na shirika la habari la reuters kwa wataalamu wa uchumi wiki hii unatoa nafasi ya asilimia 15 kwa benki kuu ya Ulaya kuanza kuchapisha fedha mwaka huu, kutokana na kuanza kwa utaratibu wa benki za juu kupata fedha kwa thamani ya chini , mpango ambao huenda utaanza mwezi Septemba.

Hakuna taarifa kuhusu Ufaransa ambayo lengo lake la mwaka 2015 la kupunguza deni la taifa lilitarajiwa kufikiwa kwa mujibu wa ukomo wa Umoja wa Ulaya wa asilimia tatu ya pato jumla la taifa. Waziri wa fedha wa Ufarabsa Michel Sapin amesema kuwa Ufaransa itapunguza nakisi kwa kasi inayostahili.

Mwandishi: Sekione Kitojo / rtre

Mhariri: Iddi Ssessanga