1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UM wapitisha azimio kusitisha hukumu ya kifo.

19 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Cdjp

New York. Baraza kuu la umoja wa mataifa limepitisha azimio ambalo halilazimiki kufuatwa kwa lazima, linalotaka kusitishwa kwa adhabu ya kifo. Azimio hilo lilipitishwa kwa kura 104 dhidi ya 54 na wajumbe 29 hawakupiga kura. Italia ikizungumza kwa niaba ya umoja wa Ulaya , imeunga mkono kwa dhati azimio hilo. Marekani, Misr, Iran na mataifa mengi ya bara la Asia yamepiga kura dhidi ya azimio hilo. Kwa mujibu wa shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International , China, Iran , Iraq , Marekani , Pakistan na Sudan zinachangia jumla ya asilimia 90 ya vifo kwa kupitia sheria hiyo duniani kote.