1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AU yasikitika Niger, Mali na Burkina Fasso, kujitoa ECOWAS

30 Januari 2024

Umoja wa Afrika umesema leo kuwa umefadhaishwa na uamuzi wa tawala za kijeshi za mataifa matatu ya Niger, Burkina Faso na Mali wa kujitoa kutoka Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS.

https://p.dw.com/p/4bqiq
Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat
Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Moussa Faki MahamatPicha: Simon Maina/AFP

Taarifa ya umoja huo imesema Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu, Moussa Faki Mahamat, amewatolea mwito viongozi wa kikanda kuongeza juhudi za mazungumzo kati ya ECOWASna watawala wa nchi hizo tatu. 

Pia umoja huo umesema uko tayari kutoa msaada wowote unaohitajika kufanikisha majadiliano yatakayosaidia kumaliza mvutano uliojitokeza kati ya jumuiya hiyo ya kikanda na mataifa hayo wanachama.

Soma pia:Nigeria yazikosoa Mali, Niger na Burkina Faso kujitoa ECOWAS

Niger, Mali na Burkina Faso zilitangaza kwa pamoja mnamo siku ya Jumapili kujiondoa ndani ya ECOWAS ikiituhumu jumuiya hiyo kukiuka misingi ya kuanzishwa kwake na kuwa kitisho kwa nchi wanachama na watu wake.