1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa kuwalinda raia wakubaliana kuendeleza hujuma za angani nchini Libya

30 Machi 2011

Marekani na Uingereza zimesisitiza hujuma za angani dhidi ya Libya zitaendelea hadi pale kanali Muamar Gaddafi atakapoyatekeleza mapendekezo ya Umoja wa Mataifa.

https://p.dw.com/p/10k8v
Washiriki katika mkutano wa LondonPicha: AP

Licha ya kuwepo kwa makubaliano mapana ya kuendelea na hatua za kijeshi, kuna migawanyiko miongoni mwa Kumuiya ya Kimataifa hasa ikiwa Kanali Gaddafi anapaswa kukubaliwa aondoke nchini Libya bila hofu ya kushtakiwa. Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Hague alipewa jukumu la kutangaza mapendekezo ya mkutano huo, na akasisitiza kuwa mataifa mengi ya Jumuiya ya Kimataifa yalikubaliana nayo.

Alisema Kongamano hilo limeonyesha kuwa wameungana katika majukumu yetu. Alisema “Tumeungana katika kutafuta Libya ambayo sio kitisho kwa raia wake, au kwa kanda au hata kwa ulimwengu mzima. Na kwa kushirikiana na walibya, wanapotafuta maisha yao ya baadaye yenye amani na thabiti“.

Uingereza imekuwa makini katika kusisitiza ushirikiano wa mataifa ya kiarabu katika kongamano hilo, Waziri Mkuu wa Qatar Sheikh Hamad aliwasilishwa kwa vyombo vya habari pamoja na william hague. Na alikuwa na ujumbe wa wazi kwake Kanali Gaddafi.

Hillary Clinton mit David Cameron in London vor Libyen Konferenz
Waziri wa nje wa Marekani Hillary Clinton na waziri mkuu wa Uingereza David CameronPicha: AP

“Tunamwomba Gaddafi na watu wake waondoke, na wasiendelee kusababisha umwagikaji damu tena. Nadhani hii ndilo suluhisho la pekee la kutatua mzozo huu haraka iwezekanavyo. Kwa sasa hatuonei dalili yoyote ya kuwepo kwa hilo, lakini matumaini haya, ambayo tunayaonyesha sasa, huenda yasiwe mezani katika siku chache zijazo“. Alisema Hamad.

Lakini hayo yanasababisha mojawapo ya migawanyiko miongoni mwa mataifa ya Jumuiya ya Kimataifa. Italia na ujerumani wamekuwa miongoni mwa nchi ambazo zinapendekeza kuwa Kanali Gaddafi anapaswa kukubaliwa kwenda uhamishoni, bila ya hofu ya kushtakiwa, kama njia ya kumaliza mgogoro huo wa Libya.

Uingereza inasisitiza kuwa ni sharti Gaddafi afunguliwe mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadam. William Hague amesema kuwa nchi yake haitajishughulisha katika kumtafutia hifadhi kiongozi huyo wa Libya.

Außenminister William Hague bestätigt britischen Militäreinsatz in Lybien
Waziri wa nje wa Uingereza William Hague(kushoto)Picha: dapd

Kongamano hilo liliafiki kuendelea kutekeleza mapendekezo ya Umoja wa Mataifa yanayolenga kuwalinda raia na kuimarisha maswala ya kiutu. Lakini Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Bibi Hillary Rodham Clinton alitangaza wazi kuwa mashambulizi ya angani yataendelea ikiwa kanali Gaddafi atayapuuza masharti ya Umoja wa Mataifa na kuendelea kuwashambulia watu wake.

Pia waakilishi kutoka kwa baraza la kitaifa la mpito nchini Libya walikutana mjini london kwa mazungumzo na viongozi wa ulimwengu na mawaziri wa mambo ya nje.

Kiongozi wa baraza hilo Guma El Gamaty aliandaa kikako na wanahabari kando na kongamano hilo na akasema matarajio ya ukweli ya watu wa Libya ni kuwa huru, kuishi chini ya mfumo wa kikatiba na demokrasia ambapo sheria itazingatiwa, uhuru wote muhimu kupewa wananchi na watu wanaweza kutimiza malengo yao.

Kongamano hilo liliwaleta pamoja wanachama wote wa wanajeshi wa muungano yaliyo nchini Libya, pamoja na Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya NATO, Umoja wa Afrika na Umoja wa nchi za Kiarabu. Urusi ilijitenga na kongamano hilo ikisisitiza kuwa hatua ya kijeshi ilizidi kile kilichoidhinishwa na Umoja wa Mataifa.

Mwandishi:Bruce Amani/DW Eng.

Mhariri: Abdul-Rahman