1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfghanistan

Umoja wa Mataifa waangazia kusitisha shuguli zao Afghanistan

11 Aprili 2023

Umoja wa Mataifa unaangazia kusitisha shughuli zake nchini Afghanistan baada ya Taliban kuwazuia wanawake kufanya kazi kwenye mashirika ya umoja huo nchini humo.

https://p.dw.com/p/4PuWD
Afghanistan Kabul | Taliban Kämpfer in der Stadt
Picha: Ebrahim Noroozi/AP Photo/picture alliance

Taarifa iliyoachapishwa mapema leo imesema, ujumbe wa Umoja wa Mataifa umesema zuio hilo la Taliban linakiuka sheria ya kimataifa na kwa maana hiyo hawakubaliani nao.

Umoja huo aidha umezionya mamlaka za Taliban  kuwa tayari kubeba mzigo utakaosababishwa na kile ilichokitaja kama mzozo kwa watu wa Afghanistan.

Taliban iliwaagiza wafanyakazi wanawake kuacha kazi kwenye mashirika hayo, isipokuwa kwa majukumu muhimu tu, ikiwa ni hatua ya karibuni zaidi katika msururu wa vizuizi dhidi ya wanawake kufanya kazi.