1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiKimataifa

Umoja wa Mataifa wakisia ukuaji duni wa uchumi wa dunia 2024

Lilian Mtono
5 Januari 2024

Umoja wa Mataifa jana Alhamisi umechapisha utabiri wa uchumi wa ulimwengu kwa mwaka 2024 inayoonyesha utaounguzwa kasi yake kutokana na majanga na mizozo.

https://p.dw.com/p/4asFa
Umoja wa Mataifa unakadiria kupungua kwa kasi ya ukuaji wa uchumi kimataifa kutokana na changamoto mbalimbali
Sehemu ya mradi mkubwa wa uzalishaji wa umeme wa kutumia nguvu ya maji katika Mto Nile unaotarajiwa kupunguza tatizo la nishati hiyo katika mataifa yanayotumia maji hayo. Picha: Minasse Wondimu Hailu/AA/picture alliance

Umoja wa Mataifa jana Alhamisi umechapisha utabiri wa ukuaji wa uchumi ulimwenguni kwa mwaka 2024, ulioonyesha utakabiliwa na changamoto zinazoanzia kwenye migogoro inayoongezeka, biashara iliyodhoofu ya kimataifa, viwango vya juu vya riba na kuongezeka kwa majanga ya hali ya hewa.

Kwenye ripoti hiyo, Umoja wa Mataifa umekadiria kuwa ukuaji wa uchumi kimataifa utapungua hadi asilimia 2.4 mwaka huu kutoka wastani wa asilimia 2.7 ya mwaka 2023.
 

Soma pia: Watafiti: Uchumi unaimarika lakini lipo ombwe kwa Wamarekani

Hata hivyo makisio hayo bado yako chini ya kiwango cha ukuaji cha asilimia 3.0 cha kabla ya mlipuko wa janga la UVIKO -19 mnamo mwaka 2020, imesema ripoti hiyo.

Utabiri huu wa Umoja wa Mataifa uko chini kuliko wa Shirika la Fedha la Kimataifa, IMF wa mwezi Oktoba na Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo, OEC uliochapishwa mwishoni mwa Novemba mwaka uliopita.