1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya huenda ukarefusha Brexit

Sekione Kitojo
23 Oktoba 2019

Rais wa baraza la Umoja wa Ulaya Donald Tusk amesema atapendekeza kwa viongozi wa umoja huo kutoa muda mwingine wa ziada  kwa ajili ya Brexit, masaa kadhaa baada ya wabunge  kukataa juhudi zake kuidhinisha Brexit. 

https://p.dw.com/p/3RlWy
Großbritanien | Boris Johnson | Unterhaus London
Picha: picture-alliance/dpa/UK Parliament/J. Taylor

Swali ni  je wanachama wengine wa  Umoja  wa  Ulaya  watakubali kuipatia  Uingereza  muda  zaidi  kujitoa  kutoka  kundi  hilo  la mataifa  kupindukia  muda  iliojiwekea  wa mwisho  wa  tarehe 31 Oktoba, na  kama  watakubali, uchelewesho  huo utakuwa  vipi?

England Brexit Parlamentssprecher John Bercow
Bunge la Uingereza likiwa katika kikao kuhusu BrexitPicha: picture-alliance/empics/House of Commons

Rais wa  baraza  la  Ulaya Donald Tusk  amesema  atayashauri mataifa  wanachama  wengine 27 kukubali  ombi  la  kuahirisha kutoka  katika  serikali  ya Uingereza, ambalo  Johnsonn amelazimishwa  kuwasilisha  siku  ya  Jumamosi  chini  ya  sheria ya  Uingereza baada  ya  kushindwa  kupata  uungwaji  mkono  wa wabunge  kwa  ajili  ya  makubaliano  yake  mapya.

Hata  hivyo , mapema  jana  Jumanne wabunge  walitoa idhinisho kwa  sheria  inayoidhinisha  makubaliano  yaliyofikiwa  kati  ya serikali  na  Umoja  wa  Ulaya  wiki  iliyopita,  na  kisha  kuzuwia muongozo wa  waziri  mkuu  wa utaratibu wa  kupitisha  makubaliano hayo  kabla  ya  muda  wa  tarehe 31 , Oktoba  wa  kujitoa  kutoka Umoja  wa  Ulaya. Boris Johnson alisema.

Albanien Tirana | Donald Tusk, Pressekonferenz mit Edi Rama
Rais wa baraz la Ulaya Doland Tusk Picha: DW/A. Ruci

"Sitakubali kabisa  kuruhusu  miezi zaidi kuhusu  hili. Iwapo bunge litakataa  kuruhusu Brexit  kutokea na  badala  yake  litaamua kuchelewesha hadi Januari ama huenda  zaidi, katika  hali  hiyo serikali  haitaweza  kuendelea  hivi. Mswada  utabidi  uondolewa na kulazimika  kuitisha uchaguzi mkuu."

Ujerumani yatoa ishara

Hata  hivyo  Ujerumani  imeonesha  kuwa  itakuwa tayari  kutoa uchelewesho wa  muda  mfupi  kwa  ajili  ya  Brexit iwapo itakuwa  ni sababu  sahihi  ya  kisiasa, amesema  hayo  waziri  wa  mambo  ya kigeni  wa  Ujerumani  Heiko Maas  katika  mahojiano  leo. Tunahitaji kufahamu,  nini  sababu   ya  hatua  hii ? Maas alikiambia kituo cha televisheni  cha  binafsi  nchini  Ujerumani  n-tv, na  kuongeza  iwapo itakuwa  juu  ya  kurudisha  tarehe  nyuma kwa  wiki  mbili  ama  tatu kuruhusu wabunge  mjini  London kutekeleza  hatua  za  kuidhinisha mswada wa  kujitoa  katika  njia  iliyo  sahihi, nafikiri  hii  haitakuwa tatizo.

Großbritanien | Boris Johnson | Unterhaus  London
Boris Johnson waziri mkuu wa UingerezaPicha: Reuters/Handout/UK Parliament/J. Taylor

Waziri mkuu wa Uingereza  Boris Johnson jana  alisema  uamuzi  ni wa  Umoja  wa  Ulaya  iwapo wanataka  kuchelewesha  Brexit  na kwa muda  gani.

Johnson amewaambia  wabunge jana baada  ya kupiga kura kukataa idhinisho la  moja  kwa  moja  la Brexit, kwamba  sera ya  serikali bado ni  kutochelewesha, na  kwamba  Uingereza inapaswa kujitoa kutoka Umoja  wa  Ulaya  Oktoba 31. Hicho ndio nitawaambia  Umoja wa Ulaya, amesema Boris Johnson.