1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya kutuma wanajeshi 1,800 Kosovo

15 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Cbxc

BRUSSELS

Viongozi wa Umoja wa Ulayawameipatia Serbia mchakato wa haraka wa kujumuishwa kwenye umoja huo.

Mpango huo ambao unaonekana kama njia ya kuendelea kulituliza eneo la Balkan wakati Kosovo ikijiandaa kujitangazia uhuru kutoka kwa Serbia tayari umekataliwa na Serbia.Viongozi wa Umoja wa Ulaya waliokuwa wakikutana mjini Brussels Ubelgiji pia wamekubaliana kimsingi kutuma kikosi cha usalama cha wanajeshi 1,800 huko Kosovo kusadia kikosi cha Umoja wa Mataifa kilioko huko hivi sasa.

Lakini hata hivyo hakuna uamuzi uliotolewa juu ya kutambuwa azma ya Kosovo wakati ikiwa njiani kujitangazia uhuru.