1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya na mazingira

27 Aprili 2007

Moshi unaochafua mazingira kutoka nchi zanachama wa Umoja wa Ulaya utaongezeka zaidi kuliko zinavyodai nchi hizo.;Kikundi ,kinachotetea mazingira-Friends of the Earth-kimegundua hayo.

https://p.dw.com/p/CHFH

Moshi unaochafua hali ya hewa, utazidi kuongezeka katika nchi za Umoja wa Ulaya na hii, licha ya madai kwamba, juhudi zinafanywa na nchi hizo kuupunguza moshi huo.

Mwezi mmoja baada ya viongozi wa Umoja wa Ulaya kuahidi kuchukua hatua kali kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa, walinzi wa mazingira wameyatuhumu mashirika muhimu ya Umoja wa Ulaya kutimiza sera ambazo mwishoe, zitaoongoza kuzidi kwa moshi huo na kuzidisha ujoto katika sayari hii.

Katika ripoti yao mpya, wachambuzi wa marafiki wa dunia hii au “FRIENDS OF THE EARTH”- wamesema mbali na kilimo misaada inayotolewa kwa nchi zisizoendelea sana na masikini za Umoja wa Ulaya ,ndio unaokula sehemu kubwa ya fedha za bajeti za Umoja huu.

Ripoti yao mpya , Friends of the Earth- inachambua matumizi ya miradi ya UU katika nchi 8 za ulaya ya kati na mashariki zilizojiunga na UU 2004,pamoja na Rumania na Bulgaria,zilizopewa mwanachama Januari mwaka huu 2007.

Katika jumla ya euro bilioni 117 zilizowekwa kando kwa nchi hizo 10 kati ya mwaka huu 2007 hadi 2013, takriban 30% zitatumika katika sekta ya usafiri.

Nchi hizo kwa kuweka usoni ujenzi wa barabara kuliko usafiri usiochafua sana mazingira kama vile reli,fedha za umma zinatumiwa kuwahimiza watu kuachana na kupanda reli na kupanda motokaa zao.

Budapest,mji mkuu wa Hungary,ni miongoni mwa miji iliopunguza fidia katika sekta ya usafiri wa umma mnamo miaka ya 1990 wakati idadi ya magari katika Jamhuri ya Czech,Slovenia na Lithuania imeshakuwa kubwa zaidi kuliko nchi iliotajiri zaidi ya Denmark.

Martin Konecny, wa shirika la marafiki wa dunia hii-FRIENDS OF THE EARTH- amesema kuwa kuna mwanya mkubwa kati ya maneno na vitendo katika sera za Umoja wa Ulaya juu ya kubadilika kwa hali ya hewa.

Hapo Machi, mwaka huu, viongozi wa dola na serikali za Umoja wa ulaya, walijitolea kupunguza moshi unaopaa hewani na kuchafua mazingira kwa kima cha 20% kuliko ilivyokua 1990 hadi ifikapo 2020.

Halafu kima hicho kitakachosalia kitapunguzwa tena kwa 30% ikiwa nchi nyengine tajiri zitawafiki –walisema viongozi hao.

Lakini, marafiki wa dunia hii wanaotetea mazingira wamesema Poland,nchi kubwa kabisa kati ya wanachama wapya wa UU ina mipango itakayoongoza kuongezeka hadi kwa kima 31% kwa moshi wake unaopaa hewani hadi ifikapo 2013 ukilinganisha na mwaka 2003.

Friends of the Earth, imegundua kuwa ni Lithuania pekee ndio iliotoa mapendekezo bora ya kutumia nishati barabara na kugeukia nishati inayoweza kutumika tena.Hii imo katika mradi wake iliotoa kwa UU ili kujipatia sehemu yake ya ruzuku.

Ingawa matumizi bora ya nishati n a matumizi ya nishati inayotumika tena kama vile jua, ni muhimu sana katika kupambana na badiliko la hali ya hewsa, Poland na Hungary zinatumia tu 1% ya msaada wao zinaopewa na UU kwa mazingira.

Akizungumza huko Stuttgart,kusini mwa Ujerumani mapema wiki hii, kamishna wa Ulaya anaehusika na sera za mikoa yake Danuta Huebner ameungama kuwa misaada anayoisimamia inabidi kupamabana na athari za badiliko la hali ya hewa.Misaada hiyo, anasema lakini, inatumiwa zaidi kupambana na athari za sera za UU zinazotokana na sekta nyengine za kiuchumi.

Banki ya UU inayotoa mikopo EIB imekosolewa halkadhalika kwa rekodi yake m baya katika sekta ya mazingira.

Bankwatch,tawi la vikundi vya watetezi wa mazingira-limetoa uchunguzi mpya juu ya fedha zipatazo dala bilioni 152 zilizotolewa na Banki hiyo kama raslimali katika miradi ya usafiri kati ya 1996-2005.

Uchunguzi huo umebainisha kwamba, banki hiyo inagharimia zaidi miradi ya usafiri inayochafua mazingira kuliko ile inayopunguza uchafuzi wake.Kwani, zaidi ya nusu ya fedha za uwekezaji za banki hiyo zimeenda katika ujenzi wa barabara na safari za ndege.

Moshi unaochafua mazingira kutoka kupanua viwanja vya ndege kulikogharimiwa na Banki hiyo kama vile uwanja wa ndege wa Heathrow,uwanja wa Amsterdam Schiphol na wa Madrid utapindukia kima cha kima mwaka cha moshi unaopaa kutoka Ireland,Norway,Slovakia,New Zealand au Uswisi viwanja hivyo vikifanya kazi kikamilifu.

Msemaji wa EIB ameieleza ripoti ya Bankwatch kuwa sawa,isipokuwa anadai imetupa macho katika sera za zamani kwani, sasa Banki hiyo imerekebisha sera zake.