1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya wapendekeza mkakati wa kuimarisha ulinzi

Sylvia Mwehozi
5 Machi 2024

Maafisa wa Umoja wa Ulaya wamezindua mkakati wa kuongeza uzalishaji na ununuzi wa silaha katika umoja huo ili kuondokana na utegemezi wa silaha za Marekani na katika kukabiliana na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4dBnX
Margrethe Vestager
Makamu wa rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya Margrethe Vestager ukiwa katika mkutanoPicha: EU/Aurore Martignoni

Makamu wa rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya Margrethe Vestager amesema muungano huo unapaswa kuchukua wajibu zaidi katika kushughulikia masuala yake ya ulinzi na kuendelea kujitolea kikamilifu kwa washirika wake wa Jumuiya ya kujihami NATO, zaidi ameongeza "Bajeti za ulinzi katika nchi zote wanachama zinapanda kwa kasi, hivyo tunapaswa kubadili njia tunayotumia. Kwa kuwa tunataka kuwekeza zaidi, tunapaswa kufanya uwekezaji bora zaidi, ambao kwa kiasi kikubwa unamaanisha kuwekeza pamoja na kuwekeza Ulaya." Miongoni mwa mikakati iliyoainishwa ni utoaji motisha kwa wazalishaji silaha wa ulaya, uwekezaji zaidi, uzalishaji wa haraka na kuorodhesha kwa pamoja kiwango cha silaha walicho nacho.