1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umwagaji damu waendelea katika Ukanda wa Gaza

1 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DGNF

GAZA:

Mashambulizi ya Israel kaskazini mwa Ukanda wa Gaza leo hii yameua Wapalestina 32 katika umwagaji mkubwa kabisa wa damu,tangu mapigano ya zaidi ya mwaka mmoja kuzuka kati ya Israel na Wapalestina katika eneo linalodhibitiwa na Hamas.Kwa mujibu wa mkuu wa huduma za dharura katika hospitali ya Gaza,Dr.Muawiy Hassanein,watoto 4 na wanawake 3 ni miongoni mwa Wapalestina waliouawa.Vile vile hadi wanamgambo 12 na wapiganaji 10 wa chama cha Hamas wameuawa.

Mashambulizi haya mapya yalianza mapema alfajiri,baada ya vifaru vya Kiisraeli vilivyosaidiwa na helikopta za kijeshi,kuvamia kambi ya wakimbizi katika mji wa Jabaliya kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.