1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Hali ya COVID-19 inatia wasiwasi chini Syria

Admin.WagnerD30 Aprili 2020

Umoja wa mataifa umeonya hali ya nchini Syria inaweza kuwa ni janga zaidi la kibinadamu kufuatia mripuko wa ugonjwa wa Corona katika nchi hiyo ambayo mfumo wake wa kiafya ni hafifu kutokana na miaka 9 ya vita.

https://p.dw.com/p/3bcbP
Syrien Damaskus Coronavirus
Picha: picture-alliance/Xinhua/A. Safarjalani

Mratibu wa masuala ya kibinadamu na misaada ya kiutu ya dharura wa umoja wa mataifa (OCHA) ameliambia baraza la usalama la umoja wa mataifa kwamba misaada ya kiutu ni lazima ipelekwe nchini Syria na kuomba mpaka baina ya Iraq na Syria ufunguliwe ili kuipeleka misaada hiyo. 

Mark Lowcock amesea kwamba tayari watu 40 wameripotiwa kuambukizwa na virusi vya Corona,huku watatu wamekufa kutokana na ugonjwa huo.

Akihutubia baraza la usalama la umoja wa mataifa, mratibu wa shirika la OCHA amesema kwamba ikiwa idadi hiyo ni ndogo kutokana na uchache wa vipimo vinavyoendeshwa nchini Syria.

Kwa upande wake mjumbe maalumu wa umoja wa mataifa kwa ajili ya Syria, aliomba usistishwaji haraka wa mapigano.

Ikiwa na mamilioni ya wakimbizi wa ndani wanaoishi katika hali ngumu na bila vyoo,ni vigumu Syria kupambana na ugonjwa huo ambao tayari ni changamoto kwa nchi tajiri.

Juhudi zinachukuliwa kujaribu kuwatenga wagonjwa

Schweiz | UN-Nothilfekoordinator Mark Lowcock | Klimawandel | Migration
Mark Lowcock, mratibu wa masuala ya kiutu wa Umoja wa Mataifa Picha: picture-alliance/Keystone/S. Di Nolfi

Juhudi zimefanywa ili kuweko na maeneo ya kuwatenga wagonjwa kwenye kambi za wakimbizi na kwenye vituo vya afya nchini humo, lakini hatua za kupambana na ugonjwa huo tayari zimesababisha athari kadhaa ikiwemo kupanda kwa bei ya vyakula kwenye baadhi ya majimbo, alisema Geir Pedersen mjumbe huyo wa umoja wa mataifa nchini Syria.

Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa umoja wa mataifa, Mark Lowcock amesema kwamba kuna umuhimu wa kufungua mpaka wa Al Yarubiyah baina ya Iraq na Syria ili kurahisisha kupelekwa misaada ya kiutu nchini humo.

Mpaka huo ulifungwa mwezi Januari kufuatia pendekezo la Urusi. Lowcock amesema kwamba misaada iliyopelekwa hadi sasa kaskazini mwa mji wa Damascus haikidhi mahitaji.

Wito wa kusitisha mapigano watolewa

Petersberger Klimadialog
Picha: picture-alliance/dpa/M. Kappeler

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guteress alitoa mwito wa usitishwaji mapigano katika maeneo yote ya vita duniani ili kupambana na ugonjwa wa COVID-19, na alirejelea mwito huo kwenye kikao cha baraza la usalama la umoja wa mataifa Jumatano.

Pedersen, mjumbe wa umoja wa mataifa nchini Syria, amepongeza kuona kwamba kumekuwa na utulivu kwenye maeneo kadhaa ya Syria na hakujashuhudiwa mapigano makubwa toka mwanzoni mwa mwezi Machi.

Amesema hadi kufikia sasa, mkataba baina ya Urusi na Uturuki na ule baina ya Uturuki na Marekani kwa ajili ya Syria inatekelezwa vyema.

Lakini alionya kwamba utulivu huo ni wa dharura na kuna uwezekano wa kuripuka upya mapigano.

Mwandishi : Saleh Mwanamilongo

Mhariri : Josephat Charo