1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Uhaba wa maji watishia mzozo wa kimataifa

John Juma
22 Machi 2023

Matumizi kupita kiasi ya maji na mabadiliko ya tabia nchi yamesababisha uhaba wa maji kuwa janga kote ulimwenguni, na kusababisha kitisho cha kutokea mzozo wa kiulimwengu.

https://p.dw.com/p/4P5WD
Pakistan | Behelfslager nach Überschwemmungen
Picha: Rizwan Tabassum/AFP/Getty Images

Tahadhari hiyo imetolewa na Umoja wa Mataifa usiku wa kuamkia leo ambayo ni Siku ya Maji Ulimwenguni.

Richard Connor, mhariri mkuu wa ripoti hiyo amesema asilimia 10 ya watu wote ulimwenguni wanaishi katika maeneo yanayokabiliwa na uhaba mkubwa wa maji.

Kulingana na ripoti hiyo ya Jukwaa la Maji la Umoja wa Mataifa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, asilimia 46 ya watu ulimwenguni kote hukosa huduma za uhakika za usafi.

Ripoti hiyo imetolewa siku moja kabla ya mkutano wa kwanza katika miaka 45 kuhusu maji, ambao umeandaliwa na Umoja wa Mataifa, mjini New York.