1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Watu 183 wameuawa tangu mwezi Julai Amhara, Ethiopia

29 Agosti 2023

Umoja wa Mataifa umesema takriban watu 183 wameuawa tangu mwezi Julai kwenye mapigano katika mkoa wa Amhara nchini Ethiopia.

https://p.dw.com/p/4VicC
Mvutano katika eneo la kaskazini mwa Ethiopia umeongezeka katika mwaka huu wa 2023.
Mvutano katika eneo la kaskazini mwa Ethiopia umeongezeka katika mwaka huu wa 2023.Picha: AP/picture alliance

Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kukomeshwa mauaji, ghasia na ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Ethiopia.

Mvutano katika eneo la kaskazini mwa Ethiopia umeongezeka katika mwaka huu baada ya kumalizika kwa vita vibaya katika mkoa wa kaskazini mwa nchi hiyo wa Tigray ambavyo pia viliwajumuisha wapiganaji kutoka mkoa wa Amhara.

Msemaji wa Ofisi ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa, Marta Hurtado, amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva kwamba Umoja wa Mataifa una wasiwasi kutokana na kuzorota kwa haki za binadamu katika baadhi ya mikoa nchini Ethiopia.