1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN yaidhinisha kikosi kipya cha AU Somalia

Bruce Amani
1 Aprili 2022

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepiga kura kwa kauli moja kupelekwa Somalia ujumbe mpya wa jeshi la kulinda amani la Umoja wa Afrika.

https://p.dw.com/p/49KFp
Somalia - Amison Soldaten  aus Burundi in Mogadishu
Picha: Getty Images/AFP/M. Abdiwahab

Wapiganaji wa Al-Shabaab wamekuwa wakiendesha harakati za kuiangusha serikali nchini Somalia kwa miaka mingi. Ujumbe wa Umoja wa Afrika nchini humo - AMISOM kwa sasa una askari 20,000, polisi na raia wanaowasaidia maafisa wa nchini humo.

Vikosi vipya vitaitwa Ujumbe wa Mpito wa Umoja wa Afrika nchini Somalia - ATMIS. Utakuwa na lengo la kuhakikisha kuwa wanajeshi wa Somalia wanachukua jukumu la usalama wa nchi yao.

Katika wiki za karibuni, taifa hilo la Pembe ya Afrika limeshuhudia wimbi la mashambulizi wakati likikabiliwa na mchakato wa uchaguzi uliocheleweshwa kwa muda mrefu.

Ujumbe wa AMISOM umekuwa Somalia kwa miaka 15 ukijaribu kujenga amani ya kudumu na usalama.