1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN yapendekeza mpango wa kuondoa vikosi vyake DRC

Saleh Mwanamilongo
30 Oktoba 2020

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amependekeza mpango, ambao utatumika kuwaondoa hatua kwa hatua wanajeshi wa kulinda amani wa umoja huo nchini Congo.

https://p.dw.com/p/3kfI9
Demokratischen Republik Kongo Beni | Monusco Fahrzeug
Picha: Getty Images/AFP/A. Huguet

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amependekeza mpango, ambao utatumika kuwaondoa hatua kwa hatua wanajeshi wa kulinda amani wa umoja huo katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na kuyakabidhi majukumu ya usalama kwa serikali ya nchi hiyo.

Katika waraka wa kurasa 15 alioliandikia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Guterres amesema ujumbe wa Umoja wa Mataifa umekubaliana na serikali ya mjini Kinshasa juu ya mkakati huo, katika mkutano wao wa tarehe 19 Oktoba, na kuongeza kuwa pande hizo zitaendelea kujadiliana, juu ya namna ya kuweka mazingira yatakayowezesha kuondoka kwa ujumbe huo.

New York António Guterres  UN-Konferenz zu Frauenrechten
Picha: UN

Katibu mkuu huyo amesema ikiwa baraza litauridhia mpango huo, Umoja wa Mataifa utaandaa mpango wa mpito, unaozingatia vigezo vya tathmini ya athari zinazoweza kuambatana na zoezi hilo, pamoja na kuainisha majukumu ya kila upande.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, nchi yenye ukubwa kuliko Ulaya magharibi, ilishuhudia machafuko na vita ambavyo vinalenga hasa rasilimali za mashariki mwa nchi hiyo. Kongo ilishuhudia pia ukoloni wa ukatili,uliofuatiwa na tawala za kidikteta. Vita vya wenyewe kwa wenyewe viliingiliwa kati na baadhi ya  nchi jirani.

Bado mpangilio wa kuondoka Monusco

Januari 2019,Kongo ilishuhudia kwa mara ya kwanza toka uhuru wake,kupeana madaraka kwa njia kidemokrasia, kufuatia kuchaguliwa kwa rais Felix Tshisekedi. Tshisekedi alichukuwa madaraka kutoka kwa mtangulizi wake Joseph kabila,kufuatia uchaguzi uliokumbwa na tuhuma za udanganyifu na kueeko na makubaliano ya siri baina ya Kabila na Tshisekedi, licha ya mgombea upinzani ambaye kulingana na matokeo yaliovujishwa kutoka tume ya uchaguzi , kwamba ndie alie ibuka mshindi wa uchaguzi huo.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa hakutoa mpangilio wowote wa kuondoka kwa kikosi hicho cha MONUSCO ambacho kina garimu kila mwaka takriban dola biloni 1.1.

Guterres amesema kwamba kuondolewa kwa vikosi hivyo kwenye majimbo matatu ya Kivu ya Kaskazini,Kivu ya Kusini na Ituri kutafanyika kwa masharti.