1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN yataka fedha kugharamia msaada wa Yemen

Oumilkheir Hamidou Mhariri: Sekione Kitojo
26 Februari 2019

Yemen  inagubikwa na mzozo mbaya kabisa kuwahi kuwasumbua binaadam ulimwenguni. Umoja wa Mataifa sasa unawasihi wafadhili wakusanye dola bilioni 4.2 kugharamia msaada wa Yemen mwaka huu.

https://p.dw.com/p/3E6Yv
UN Sicherheitsrat Yemen
Picha: Reuters/C. Allegri

Umoja wa Mataifa unawasihi wafadhili wakusanye dola bilioni 4.2 kugharamia msaada wa Yemen kwa mwaka huu. Wayemen milioni 20 wanasumbuliwa na uhaba wa chakula. 

"Yemen  inagubikwa na mzozo mbaya kabisa kuwahi kuwasumbua binaadam ulimwenguni"  maafisa wa Umoja wa Mataifa wamesema  mnamo wakati ambapo mkutano wa wafadhili wa kimataifa unatarajiwa kuitishwa hii leo mjini Geneva na kuongeza kusema takriban  watu 250.000 wabnasumbuliwa  vibaya sana na njaa baada ya miaka minne ya vita.

Fedha ambazo Umoja wa Mataifa unataraji kukusanya hazikulengwa pekee kuwapatia misaada ya chakaula watu milioni 12 kwa mwaka huu, idadi ambayo ni sawa na thuluthi moja ya wakaazi jumla wa Yemen, bali pia kuwapatia maji safi ya kunywa, madawa na kugharamia shughuli za kilimo.

Watoto wengi wanakabiliwa na changamoto ya utapia mlo
Watoto wengi wanakabiliwa na changamoto ya utapia mloPicha: picture-alliance/AP Photo/H. Mohammed

Watoto wanasumbuliwa zaidi na utaapia mlo.Fatima ni msichana wa miaka 12 ana uzito wa kilogram kumi tu.Amebakia mifupa mitupu. Babaake Hadi Ibrahim ameeleza kuwa:

"Sababu ya hali hii ni kuhama hama kutokana na mapigano.Tulikuwa tunaishi chini ya mti. Nimeacha kila kitu nilichokuwa nacho na kukimbia mauti kutokana na mashambulio ya ndegeb za kivita. Hiyo ndio sababu hakuwa akipata chakula na kushikwa na maradhi. Nafanya kila niwezalo, nampeleka hospitali moja baada ya nyengine, bila ya kufanikiwa."

Mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia watoto UNICEF, kanda ya Mashariki ya Kati, Gerrt Cappalaere anasema watoto milioni moja na laki mbili wanaishi katika maeneo ya vita nchini Yemen na wengi wao wanasumbuliwa na utapia mlo na hawapati matibabu.

Ukosefu wa maji safi na salama umetajwa kuwa miongoni mwa changamoto kwa Wayemen
Ukosefu wa maji safi na salama umetajwa kuwa miongoni mwa changamoto kwa WayemenPicha: Reuters/K. Abdullah

Mkutano wa wafadhili wa Yemen mjini Geneva unalenga kukusanya dola bilioni 4.2. Wa mwaka jana ulipelekea kukusanywa asili mia 83 ya dala bilioni 3 zilizoshauriwa na Umoja wa mataifa. Wafadhili mkuu mwaka jana walikuwa Saudi Arabia na falme za nchin za kiarabu ambao ni miongoni mwa nchi zinazounga mkono serikali ya Yemen dhidi ya waasi wa Houthi wenye mafungamano kwa upande wao na Iran.

"Tunataka kuona unafiki  wa mataifa yanayofanya biashara ya silaha au yale yanayodondosha makombora na mizinga nchini Yemen unakoma" anasaema Jan Egeland,ambae ni mkuu wa baraza la Norway linalaoshughulikia wakimbizi-taasisi inayoshirikiana na mashirika ya umoja wa mataifa nchini Yemen.

Vyanzo: dpa