1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

UNCEF yasema watoto 17,000 Gaza hawana ndugu wa karibu

Iddi Ssessanga
3 Februari 2024

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF, limesema watoto wapatao 17,000 kwa Kipalestina na vijana wanaishi bila wazazi wao au ndugu katika Ukanda Gaza.

https://p.dw.com/p/4bzmD
Gaza- wakimbizi watoto.
UNICEF imesema maelfu ya watoto Gaza hawako na wazazi au ndugu zao wa karibu.Picha: MAHMUD HAMS/AFP

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF, limesema watoto wapatao 17,000 kwa Kipalestina na vijana wanaishi bila wazazi wao au ndugu katika Ukanda Gaza, ambao unakabiliwa na mashambulizi ya Israel tangu Oktoba 7, kufuatia uvamizi wa Hamas kusini mwa Israel, uliosababisha vifo vya zaidi ya watu 1,200.

Idadi ya watu waliokufa Gaza imefikia 27,131, wengi wao wakiwa wanawake, watoto au vijana, huku 66,287 wakiwa wamejeruhiwa. Msemaji wa UNCEF katika kanda hiyo Jonathan Crickx, amesema wazazi wa watoto hao ama wameuawa, kujeruhiwa au walilaazimika kuhamia kwingine.

Soma pia: UN: Wanawake na watoto ndio waathirika wakubwa katika vita ukanda wa Gaza

Wakati huo huo, waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock ameionya Israel dhidi ya kutanua operesheni yake katika mji wa Rafah, kusini mwa Gaza, na kusema hatua hiyo haitakuwa na uhalali wowote.

Waziri Baerbock amesema Ujerumani na Marekani zimeweka wazi kwa Israel kwamba wakaazi wa Gaza hawawezi kuondoshwa kwenye makaazi yao.

Kauli hiyo imefuatia ripoti zilizomnukuu waziri wa ulinzi wa Israel Yoav Galant, akisema Alhamisi kwamba watatanua operesheni Rafah kuzikabili brigedi za Hamas huko.