1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Watoto wapatao 300 waokolewa Khartoum nchini Sudan

Tatu Karema
8 Juni 2023

Watoto wapatao 300, miongoni mwao wakiwamo wachanga wameokolewa kutoka kituo cha mayatima kilicho katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum.

https://p.dw.com/p/4SKev
Tödliches Waisenhaus im Sudan
Picha: Nazim Sirag/AP/picture alliance

Matukio ya kuhuzunisha katika kituo hicho cha Al-Mayqoma yaligonga vichwa vya habari mwishoni mwa mwezi uliopita, wakati mapigano makali baina ya jeshi rasmi la serikali na wanamgambo wa RSF yalipokuwa yakirindima katika eneo linalokizunguka kituo hicho cha watoto yatima.

Madhila ya raia wa Sudan yamulikiwa 

Vifo vya watoto vilimulika madhila wanayoyapitia raia wa Sudan tangu uhasama wa kivita uliozuka kati ya jeshi linaloongozwa na Jenerali Abdel-Fattah Burhan na wanamgambo wa RSF wanaoongozwa na Jenerali Mohammed Hamdan Dagalo katikati mwa mwezi Aprili.