1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaMorocco

UN: Watoto 100,000 wameathiriwa na tetemeko la ardhi Morocco

14 Septemba 2023

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia watoto UNICEF, limesema watoto takriban 100,000 wameathiriwa na tetemeko la ardhi lililoikumba nchi hiyo wiki iliyopita na kusababisha vifo vya karibu watu 3000.

https://p.dw.com/p/4WJHB
Marokko nach dem schwerem Erdbeben
Picha: Hannah McKay/REUTERS

Idadi kubwa ya familia zimekosa makazi na hulazimika kulala nje wakati huu wa baridi kali.

Shirika la Msalaba Mwekundu la Ujerumani (DRK) limesema litatuma  nchini Morocco Alhamisi hii shehena ya kwanza ya tani 37 za vifaa vya msaada. Juhudi za uokozi zinaendelea hadi leo hii nchini humo licha ya matumaini hafifu ya kuwapata manusura.

Serikali ya Morocco imekuwa ikikabiliwa na shinikizo kubwa la kukubali msaada zaidi wa kimataifa. Lakini hadi sasa, taifa hilo la Afrika Kaskazini limeafiki rasmi msaada kutoka nchi nne ambazo ni Uhispania, Uingereza, Qatar na Umoja wa Falme za Kiarabu.