1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Unyanyasaji wa kingono waongezeka mjini Goma, DRC

Sudi Mnette
10 Mei 2023

Shirika la Madaktari wasio na mipaka MSF limesema kumekuwa na ongezeko la visa vya unyanyasaji wa kijinsia karibu kila siku katika mji wa mashariki wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wa Goma.

https://p.dw.com/p/4R7vW
Mama huyu aliyeyakimbia makazi yake kutokana na mashambulizi huko Goma aliyofanya kuondoka maeneo yao.
Mashambulizi ya makundi yenye silaha yamekuwa yakisababisha changamoto nyyingi nchini Jahmuri ya Kidemokrasia ya Kongo na hasa ya kijamii.Picha: DW

Kulingana na shirika hilo la MSF, kuanzia Aprili 17 hadi 30, limekuwa likiwasaidia waathirika wapya 48 kwa siku na hasa katika maeneo ambayo watu wamekimbia makazi yao katika mji mkuu huo wa jimbo lenye migogoro la Kivu Kaskazini. Shirika hilo MSF limeongeza kwa kusema takriban asilimia 60 ya visa hivyo vinahusisha wanawake ambao walivamiwa katika muda wa saa 72 zilizopita. Jason Rizz ambaye ni mratibu wa matukio ya dharura katika shirika MSF amesema kwa miezi kadhaa wamekuwa wakishughulikia idadi kubwa ya matukio ya unyanyasaji wa kijinsia lakini haijawahi kufikia kiwango cha juu kama ilivyo katika majuma ya hivi karibuni nchini humo.