1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Upinzani Kenya watishia kufanya maandamano

7 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D3g0

NAIROBI:

Chama cha upinzani cha ODM nchini Kenya kimetishia kufanya maandamano zaidi iwapo serikali itakutana na Jumuiya ya IGAD.Mkutano huo umepangwa kufanywa leo hii mjini Nairobi.Rais Mwai Kibaki wa Kenya hivi sasa ni mwenyekiti wa jumuiya hiyo ya madola saba.Chama cha upinzani kina hofu kuwa mkutano huo utakuwa njia ya kumuidhinisha Kibaki kama rais kupitia mlango wa nyuma.Chama cha ODM kinasema hakijashauriwa kuhusu mkutano huo na huenda ukahatarisha mazungumzo ya upatanisho yanayoendelea hivi sasa chini ya usimamizi wa aliekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan.