1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Upinzani mkali dhidi ya serikali Ujerumani

9 Juni 2010

Umejitokeza upinzani mkubwa kutoka vyama vya upinzani, vyama vya wafanyakazi na vyama vya kijamii dhidi ya hatua ya kubana matumizi ambayo imetangazwa na serikali ya Ujerumani siku Jumatatu

https://p.dw.com/p/NmFz
Kansela wa Ujerumani Angela MerkelPicha: AP

Kiongozi wa muungano wa vyama vya wafanya kazi nchini Ujerumani , Michael Sommer, ametangaza hatua za upinzani dhidi ya mipango ya kupunguza mafao ya kijamii. Hatua ya serikali ya kubana matumizi kuanzia mwaka 2011 hadi 2014 ina lengo la kupunguza kiasi cha Euro bilioni 80.

Upande wa upinzani unauona mpango wa serikali wa kubana matumizi kuwa ni wa maangamizi. Mpango huo wa kubana matumizi, kwa upande mmoja, unalenga kwa wale walio katika hali dhaifu kijamii, amekosoa kiongozi wa chama cha Social Democratic, SPD Sigmar Gabriel.

´´Kile kilichopo hapa ni matokeo ya kubuni, ambayo lakini yataweka mbinyo kwa wafanyakazi pamoja na familia zao. Hakuna mantiki yoyote hapa, haionyeshi kama Ujerumani itaweza kujitoa kutoka katika mzozo huu, badala yake kile serikali ya Ujerumani ilicholeta baada ya miezi minane kuwapo madarakani ni mateso matupu´´

Kile alichokikosoa kiongozi wa chama cha SPD, Sigmar Gabriel, ndicho pia alichosema kiongozi wa chama cha walinzi wa mazingira , The Greens, Claudia Roth, kwamba wale wenye kipato cha juu hawataguswa na mpango huu wa kubana matumizi.

´´Nani atabeba mzigo huu iwapo hakutakuwa na mafanikio, basi inabidi pia kuwajibika zaidi. Kwa mfano, kwa kupandisha kodi ama kutoza kodi baadhi ya mali´´

Kiongozi wa kundi la wabunge wa chama cha Die Linke katika bunge la Ujerumani, Bundestag, Gregor Gysi, analiangalia tatizo hilo kuanzia kileleni.

Serikali ya Ujerumani leo imeamua kuuvunja mfumo wa soko huru. Na ni matumaini yangu, kwamba hii inapanua zaidi upinzani wa umma dhidi yao.

Tayari vyama kadha vya kijamii, kama Shirikisho la vyama vya wafanyakazi wa Ujerumani, vimetangaza nia hiyo. Kiongozi wa shirikisho hilo, DGB, Michael Sommer, amekwisha tangaza mapambano dhidi ya serikali ya Ujerumani pamoja na vyama vinavyounda serikali ya mseto.

´´Hii si serikali ya mrengo wa kati, hii ni serikali ya watu wenye kipato cha juu na matajiri´´

Waziri wa masuala ya jamii, Ursula von der Leyen, anatetea hatua hiyo ya kubana matumizi katika eneo lake, kwamba eneo hilo ndio limesababisha kwa kiasi kikubwa hali hii ya kitaifa. Hata baadhi ya wanasiasa wanaotetea masuala ya kijamii kutoka chama cha Christian Democratic , CDU, wanadai kuwa wale wenye kipato cha juu waongezewe kodi ya mapato .

Mwandishi : Stützle, Peter / ZR / Sekione Kitojo.

Mhariri: Miraji Othman