1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ureno yajiandaa kupeleka wanajeshi wake Msumbiji

Saleh Mwanamilongo
30 Machi 2021

Ureno imesema itapeleka wanajeshi nchini humo mapema mwezi Aprili baada ya wanamgambo wenye itikadi kali kuushambulia mji wa Palma.

https://p.dw.com/p/3rOl8
BG I Alltag und Militarismus in Cabo Delgado
Picha: Roberto Paquete/DW

Wanajeshi hao wa Ureno watakuwa na jukumu la kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa Msumbiji, hayo ni kwa mujibu wa shirika la habari la Lusa ambalo limenukuu chanzo kutoka wizara ya ulinzi. Shirika hilo la habari la Ureno limesema makubaliano ya pande hizo mbili yanahusu kikosi maalum cha  Ureno cha wanajeshi 60 watakaopelekwa Msumbiji.

Wanamgambo hao wanaodai kuwa na mafungamano na kundi la kigaidi linalojiita Dola la Kiislam waliushambulia mji wa bandari wa Palma Jumatano iliopita. Waliharibu majengo na kuwauwa raia wengine kwa kuwakata vichwa. Watu walionusurika walikimbilia kwenye mji jirani wa Mueda na kwenye mji mkuu wa jimbo hilo, Pemba.

Mkurugenzi wa kampuni binafsi ya usalama,DAG,Max Dyck amesema mapigano yaliyoanza Jumatano wiki iliyopita bado yanaendelea. Kadhalika duru zimearifu kwamba maelfu ya wakaazi wa Palma bado wamekwama katika mji huo  wakihangaika kutafuta njia ya kuondoka kutoka kwenye mji huo unaoshikiliwa na wapiganaji hao.

Wanamgambo wauendelea kushikilia mji wa Palma

Wengi wamekimbilia msituni kuelekea eneo la kaskazini kwenye mpaka na nchi jirani ya Tanzania. Mamia wengine walielekea kwenye ziwa la Afungi, eneo ambako kunazalishwa gesi na kampuni ya Ufaransa ya Total.

Mashirika ya misaada yameelezea wasiwsai wao kuhusu hali ya raia wa Palma, mji ambao mawasiliano yamekuwa magumu.

Raia wamejihami kwa silaha dhidi ya wanamgambo mjini Mueda, jimboni Cabo del Gado.
Raia wamejihami kwa silaha dhidi ya wanamgambo mjini Mueda, jimboni Cabo del Gado.Picha: Roberto Paquete/DW

Mjini Pemba, wafanyakazi wa mashirka ya misaada wamekuwa wakipokea wakimbizi. Padre Kwiriwi Fonseca alieko kwenye mji wa Pemba amesema wengi ya wakimbizi wamekuja na mejeruhi na walifichama kwa zaidi ya siku nne na hawana chakula.

Manusura wamekuwa wakiwatafuta ndugui zao ambao wamepotea. Mji wa Pemba unawapokea mamia ya maelfu ya wakimbizi. Toka kuanza kwa machafuko hayo,watu laki saba wamaeyahama makaazi yao.

Dola la Kiislamu ladai kuhusika na mashambulizi ya mjini Palma

Raia wa Palma wakimbia mji huo baada ya wanamgambo kuuteka Jumatano.
Raia wa Palma wakimbia mji huo baada ya wanamgambo kuuteka Jumatano.Picha: Alfredo Zuniga/AFP/Getty Images

 Shambulizi la Palma ndio kubwa toka kundi hilo la wanamgambo kuanza mashambulizi kwenye eneo hilo la kaskazini mwa Msumbuji mwaka 2017.

Zaidi ya watu 2600 nusu wakiwa raia wameuliwa kwenye mashambulizi ya wanamgambo hao wenye mafungamano na Dola la Kiislam.

Umoja wa Mataifa umelezea kwamba mapigano ya hapa na pale yalishuhudiwa asubuhi ya leo juma nne kwenye mji huo wa Palma.

Jana, kundi linalojiita Dola la Kiislamu limedai kuwa wapiganaji wake ndio wamehusika na mashambulizi katika mji wa Palma.