1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi washangazwa kuanguka kwa ukuta

3 Novemba 2009

<p>Ukuta ulipoporomoka miaka 20 iliyopita,watu wote waliduwaa.Urusi pia.Katibu mkuu Mikhael Gorbatschow alikawia kuarifiwa.

https://p.dw.com/p/KIJj
Mauerfall 1989 Mauer Berlin grenztruppen DDR ** FILE ** East German border guards look through a hole in the Berlin wall after demonstrators pulled down one segment of the wall at Brandenburg gate in this November 11, 1989 file picture. 2009 marks the 20th anniversary of the fall of the Berlin Wall. (AP Photo/Lionel Cironneau, File)
Ukuta waangushwa katika lango la Brandenburg tarehe 11 Novemba,1989Picha: AP
Hakuna aliyeweza kuashiria hali ya mambo katika Jamhuri ya kidemokrasi ya Ujerumani -GDR-ingechukua sura gani -hata shirika la upelelezi la KGB halikuweza.Roman Goncharenko amezungumza na walioshuhudia tukio hilo.

Jumatatu ya November tisa mwaka 1989,balozi wa Urusi katika jamhuri ya kidemokrasi ya Ujerumani-GDR,Wjatscheslaw Kotschemassow alitaka kumpigia simu mkubwa wake,waziri wa mambo ya nchi za nje Edouard Schewardnadse.Hali inatisha:Serikali ya Berlin Mashariki inataka kuwarahisishia shughuli za usafiri wananchi wake waweze kuingia Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani na anataka kujua kama Usovieti haina pingamizi.Mjini Moscow lakini hakuna anaejibu simu:

Sababu kwamba hakuna anaejibu simu pengine inatokana na ile hali kwamba siku chache kabla watu nchini Soviet Union walikuwa wakisherehekea miaka 72 ya mapinduzi ya October.Viongozi wa serikali hawapatikani.Naibu waziri wa mambo ya nchi za nje,ambae hakuwa akijua cha kufanya,akaruhusu,wafanye kile wanachotaka kufanya "marafiki zao" kama wenyewe Warusi na Wajerumani mashariki walivyokuwa wakijiita zamani.

Magharibi ilipowadia,watumishi wa ubalozi wa Urusi wakafuatilizia katika televisheni mkutano aliokuwa nao Günter Schabowski pamoja na waandishi habari.Walishtuka walipomsikia mwanachama huyo wa kamati kuu ya kisiasa akitangaza kufunguliwa ukuta.Kwa sababu ruhusa ya Moscow ilihusiana na kuvuka mpaka wa Ujerumani tu kuingia Jamhuri ya Tcheki.

"Nijuavyo mie,ruhusa hiyo inaanza tangu sasa."

Hapo ikazuka hali ambayo kwa mtazamo wa leo mtu anaweza kusema si ya kawaida.Badala ya kumuarifu moja kwa moja katibu mkuu wa chama cha kikoministi cha Usovieti-Mikhael Gorbatchov,balozi wa Usovieti aliyeonyesha amechoka, Kotschemassow,akaamua kumeza vidonge vya usingizi-na kulala hapo hapo.Saa chache baadae,maelfu ya wajerumani mashariki walipoanza kuongozana kuingia Berlin Magharibi,msaidizi wake Igor Maximiytschew alijikuta akikabiliwa na kizungumkuti kikubwa:kimsingi alilazimika kuwapigia simu viongozi wa Kremlin na kwa namna hiyo kusababisha jibu la pupa.Maximytschev akawakumbuka wale ambao walipendelea zaidi ufumbuzi wa kichina,yaani jeshi liingilie kati na kutumia nguvu kama ilivyotokea katika uwanja wa Tiananmen, mjini Beijing,miezi michache kabla,ili kulivunja nguvu vuguvugu la waliokuwa wakidai demokrasia.Ingawa Gorbatschov aliondoa uwezekano kama huo,lakini simu ya kutoka Berlin,tena saa za usiku,ingeangaliwa kama ishara mambo yanatisha.Balozi wa Urusi lakini aliamua vyengine.

Hata watumishi wa idara ya upelelezi ya Urusi waliduwaa.Iwan Kusmin alikuwa wakati ule, mkuu wa idara ya habari ya KGB.Yeye aliangalia televisheni na kuona mkutano wa Shabowski pamoja na waandishi habari.Lakini alifikiri hauna umuhimu mkubwa,akenda kulala.Aliamshwa saa sita za usiku na maafisa wa makao makuu ya KGB ya Berlin-Karlshorst na kuarifiwa kwamba mipaka imefunguliwa.

Mwandishi:Gonscharenko,Roman/Hamidou Oummilkheir

Mhariri:Abdul-Rahman